Jumatano, 2 Desemba 2015

TAMBI ZA SPAGHETTINI NA KUKU

MAHITAJI
1.Tambi za spaghettini pakti 1
2.Kuku nusu
3.Nyanya (Tungule) kubwa 3
4.Pilipili hoho(pilipili boga) 1
5.Karoti kubwa 1
6.Mafuta kiasi
7.Tangawizi iloswagwa kijiko cha chakula 1
8.Kitunguu thomu kilosagwa kijiko 1
9.Royco(Ukipenda) kijiko 1
10.Chumvi kiasi
11.Kitunguu maji
12.Maji kiasi

MAANDALIZI
1.Kata kata vipande vyako vya kuku upendavyo
2.Muoshe kisha muweke pembeni
3.Kata kata Pilipili hoho na keroti kwa umbo la pembe nne(square)
4.Kata kata vitunguu maji weka pembeni
5.Para au saga nyanya zako weka pembeni
6.Vunja tambi zako weka pembeni

JINSI YA KUPIKA 
1.Muweke kuku wako tangawizi,kitunguu thomu na chumvi
2.Kisha muweke jikoni mwache kidogo kisha weka maji
3.Chemsha kuku wako mpaka aive
4.Weka maji jikoni mpaka yachemke kidogo
5.Weka tambi zako zikiiva zichuje maji ziweke pembeni
6.Weka sufuria kavu na weka mafuta kwa ajili ya kukaanga
7.Anza kukaanga vitunguu maji kisha pilipili hoho na malizia na karoti
8.Weka nyanya acha dakika 1 kisha weka chumvi kiasi
9.Mimina nyama yako ya kuku koroga acha dakika 2 kisha onja kama chumvi ipo sawa malizia kwa kuweka tambi
10.Changanya tambi vizuri subiri kidogo zikauke ule mchuzi ubaki kidogo sana
Angalizo:
1.Hakikisha tambi huzichemshi mpaka zikavurugika
2.Usimimine tambi kama mchuzi haujapungua
3.Usikaushe tambi zako kabisa kabisa acha zikiwa na rosti kwa mbali

Furahia Tambi Zako.

2 comments:

Emmanuel Matem alisema ...

Inaonekana Tamu sana,sante.

Unknown alisema ...

Asante

Chapisha Maoni