Alhamisi, 10 Desemba 2015

KUKU LAINII WA KUKAANGA(FRIED SOFT CHICKEN)


MAHITAJI
1.Kuku nusu(Vidali 2)
2.Chumvi kijiko 1
3.Pilipili ya unga kijiko 1
4.Pilipili Manga nusu kijiko
5.Blue band kijiko 1
6.Mtindi robo kikombe
7.Mafuta nusu lita
8.Chicken Masala kijiko 1
9.Tangawizi ya unga kijiko 1

MAANDALI
1.Muoshe kuku vizuri na muweke kwenye bakuli safi
2.Weka blue band kwenye frying pan iache iyayuke  
3.Muweke pilipili,chumvi,pilipili manga,blue band,mtindi,masala na tangawizi kisha mchanganye vizuri
4.Muweke kwenye friji akolee viungo kwa lisaa

JINSI YA KUPIKA
1.Weka mafuta kwenye karai na uyaweke jikoni
2.Acha yapate moto kiasi kisha weka kuku wako
3.Mwache aive mpaka afanye rangi ya brown
4.Kisha mgeuze upande mwengine
5.Endelea kumpika mpaka nyama yote iwe brown
6.Epua muweke kwenye tissue au chujio
7.Akipoa huyu kuku huwa mlainii na mtamu unaweza kula na chipsi,wali,mkate au chochote upendacho
Angalizo:
1.Usimpike sana hadi kukauka
2.Usiweke kuku kama mafuta hayajapata moto vizuri

Furahia Kuku Wako.




0 comments:

Chapisha Maoni