Jumanne, 22 Desemba 2015

VANILLA MILK SHAKE






MAHITAJI
1.Ndizi mbivu 2
2.Maziwa pakti 1
3.Sukari kijiko cha chakula 1
4.Arki Vanilla kijiko cha chai 1
5.Custard kijiko cha chakula 1
9.Vipande vya barafu

MAANDALIZI
1.Osha ndizi zikiwa na maganda yake vizuri
2.Menya ndizi na uikate kisha weka kwenye jagi la blender
4.Mimina maziwa kwenye ndizi
5.Weka sukari,custard na arki
6.Malizia kuweka barafu zako

JINSI YA KUTENGENEZA
1.Chukua jagi weka kwenye blender
2.Kisha saga mchanganyiko huo kwa dakika kadhaa
3.Rudia kusaga kwa mara ya pili ikisagika vizuri mimina kwenye gilasi
4.Chukua mrija tayari kwa kunywa
Angalizo:
1.Kama huna barafu saga na maziwa ya baridi
2.Ukipenda ya baridi sana weka kwenye friji
3.Kama mchanganyiko mzito sana weka maji kidogo
4.Sio lazima kuweka sukari

Furahia Kinywaji Chako.

0 comments:

Chapisha Maoni