Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Salad. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Salad. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 3 Desemba 2015

MATUNDA(FRUITS)

MAHITAJI
1.Parachichi vipande 2
2. Nanasi vipande 2
3.Papai vipande 2 
4.Tikiti maji vipande 2 
5.Ndizi vipande 2 
6.Tango vipande 2 
7.Karoti vipande 2 
8.Embe vipande 2 

JINSI YA KUANDAA
1.Chukua sahani uipendayo
2.Kata kata kila tunda vipande viwili umbo upendalo
3.Panga kwenye sahani yako kwa muonekano wa kuvutia
4.Unaweza tumia Uma au tooth pick kula matunda yako 
Angalizo:
1.Osha matunda vizuri kabla ya kuyandaa 
2.Andaa matunda yako kwa usafi wa hali ya juu
3.Vizuri kula matunda dakika 10 kabla au baada ya kula chakula

Furahia Matunda Yako
 

Jumamosi, 21 Novemba 2015

SALAD


MAHITAJI
1.Vitunguu maji 3
2.Tango kubwa 1
3.Nyanya kubwa 3
4.Karoti 1
5.Pilipili boga(Pilipili hoho) 1
6.Ndimu 1
7.Chumvi

MAANDALIZI
1.Osha Vitu vyako nilivyo taja hapo juu 
2.Kisha kata kata vitu vyako kwa shape upendayo na uviweke mbali mbali yaani kila kitu na sehemu yake
3.Chukua vitunguu maji vioche na chumvi
4.Chukua kipario(Grater) para karoti yako
5.Kata pilipili hoho nyembamba nyembamba

JINSI YA KUTENGENEZA
1.Chukua chombo chako safia cha kuweka salad yako
2.Anza kupanga Vitunguu maji chini
3.Kisha weka keroti
4.Kisha weka pilipili hoho
5.Kisha weka nyanya
6. Malizia kuweka na Tango
7.Nyunyizia chumvi juu
8.Malizia Kunyunyizia Ndimu ulio ikamua

NB: 1.Unaweza kupamba kwa design uipendayo ili ivutie
         2.Unaweza kuengezea vitu zaidi kama pilipili,Vinegar
         3.Unaweza kula na Pilau,Chipsi,Wali ama chochote.

Furahia Salad Yako.