Jumamosi, 21 Novemba 2015

SALAD


MAHITAJI
1.Vitunguu maji 3
2.Tango kubwa 1
3.Nyanya kubwa 3
4.Karoti 1
5.Pilipili boga(Pilipili hoho) 1
6.Ndimu 1
7.Chumvi

MAANDALIZI
1.Osha Vitu vyako nilivyo taja hapo juu 
2.Kisha kata kata vitu vyako kwa shape upendayo na uviweke mbali mbali yaani kila kitu na sehemu yake
3.Chukua vitunguu maji vioche na chumvi
4.Chukua kipario(Grater) para karoti yako
5.Kata pilipili hoho nyembamba nyembamba

JINSI YA KUTENGENEZA
1.Chukua chombo chako safia cha kuweka salad yako
2.Anza kupanga Vitunguu maji chini
3.Kisha weka keroti
4.Kisha weka pilipili hoho
5.Kisha weka nyanya
6. Malizia kuweka na Tango
7.Nyunyizia chumvi juu
8.Malizia Kunyunyizia Ndimu ulio ikamua

NB: 1.Unaweza kupamba kwa design uipendayo ili ivutie
         2.Unaweza kuengezea vitu zaidi kama pilipili,Vinegar
         3.Unaweza kula na Pilau,Chipsi,Wali ama chochote.

Furahia Salad Yako.

0 comments:

Chapisha Maoni