Jumatano, 18 Novemba 2015

TAMBI ZA KUKAANGA



MAHITAJI
1. Tambi Nyembamba Pakti 1
2. Sukari Glasi Ndogo1
3. Hiliki Kiasi
4. Arki Vanilla Kijiko 1
5. Zabibu Kavu Kiasi
6. Mdalasini mzima kiasi   
7. Mafuta Ya Kukaangia Robo Kikombe
8. Maji Glasi Kubwa 2

MAANDALIZI
1.      Pasua tambi zako weka pembeni
2.      Menya hiliki kisha zitwange

JINSI YA KUPIKA
1.Weka mafuta kwenye sufuria anza kukaanga tambi zako mpaka ziwe na rangi ya brown
2. Kisha weka maji,hiliki,sukari,mdalasini,zabibu na arki vanilla
3. Koroga kidogo kuchanganya tambi zako
4. Funika acha zichemke mpaka zikauke
5. Zikikauka funika na mkungu weka mkaa juu yake kama unavyo pika wali acha zikauke vizuri
6. Baada ya dakika 10 epua.
7. Changanya vizuri kisha pakua.


Angalizo: 

1.Ili tambi ziwe nzuri hakikisha maji hayawi mengi ili ziweze kuchambuka.
2.Unaweza kuongeza sukari kama mpenzi wa sukari

Furahia Tambi Zako
                    

2 comments:

Unknown alisema ...

Ntafanyaje zikiwa ngumu

Unknown alisema ...

Ntafanyaje zikiwa ngumu

Chapisha Maoni