Jumatatu, 30 Novemba 2015

UGALI SAMAKI


MAHITAJI
1.Samaki umpendae
2.Pilipili ya kuwasha 1
3.Vitunguu thomu punje2
4.Chumvi kiasi
5.Ndimu 1 kubwa
6.Mafuta kikombe kikubwa 1
7.Unga wa sembe robo
8.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Osha Samaki wako baada ya kumpara na kuondoa Maganda yote
2.Mkate Kate au mpasue tu ili aweze kuingia Viungo vizuri
3.Twanga Pilipili, Kitunguu thomu na Chumvi kisha weka kwenye Samaki wako
4.Mkamulie Ndimu kisha muache kwa dakika 30 au zaidi ako lees Viungo ukipenda muweke kwenye fridge
5.Chunga Unga wako wa ugali weka pembeni
6.Weka maji kiasi kwenye sufuria ndogo unayo taka kusongea ugali wako
7.Chukua kibakuli weka maji kisha chota Unga miko miwili na ukoroge kama unataka kupika uji
JINSI YA KUPIKA UGALI
1.Weka maji jikoni acha yapate moto kidogo
2.Mimina uji ulioukoroga pembeni kwenye sufuria yako
3.Koroga hakikisha uji sio mwepesi sana wala mzito sana
4.Acha uchemke mpaka utokote kisha anza kuweka Unga mkavu kidogo kidogo huku ukiukoroga
5.Songa ugali wako kwa dakika 4 kisha acha kidogo utulie
6.Endelea kuusonga tena mpaka uwe mlaini kwa dakika 5
7.Ufunike kidogo kwa dakika moja kisha pakua
8.Weka kwenye sahani au hot pot
9.Kula na Samaki, kachumbari, Maharage, Mchuzi, Nyama 'n.k. 
JINSI YA KUPIKA SAMAKI
Kuna njia mbili: Unaweza kumkaanga au kumchoma
1.Kukaanga weka frying pan au karai jikoni weka mafuta
2.Yakipata moto muweke samaki wako
3.Baada ya dakika 4 mgeuze upande wa pili
4.Muwache aive upande mwengine kisha mtoe
5.Muweke kwenye tissue au chujio achuje mafuta
6.Akipoa tayari kwa kula
7.Hakikisha moto ni wa wastani usiwe mdogo wala mkubwa
8.Usiweke samaki kwenye mafuta mpaka yapate moto kisawa sawa
Ama kwa kumchoma
1.Chukua wavu wa kuchomea samaki au nyama
2.Weka samaki wako mwache kwa dakika 1 kisha mpake mafuta
3.Hakikisha moto ni mdogo kiasi ili asiungue
4.Baada ya dakika 5 mgeuze upande wa pili na mpake tena mafuta
5.Msubiri kwa dakika 5 nyengine kama kaiva mtoe

 NB: 1.Ili ugali uwive hakikisha maji yanachemka vizuri
         2.Jitahidi kuusonga vizuri ili uwe mlaini
         3.Tumia mwiko wa ugali kusongea ugali

Furahia Ugali na Samaki Wako.
posted from Bloggeroid

0 comments:

Chapisha Maoni