Ijumaa, 10 Juni 2016

JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI/HOW TO COOK SOFT CHAPATI


JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI

MAANDALIZI/PREPARATION
1.Kwanza hakikisha unakanda unga vizuri
 Make sure you knead the dough very well

2.Lazima unga uukande mpaka uwe laini sana
  The kneaded dough must be very soft

3.Baada ya kukata madonge ya idadi ya chapati unazo zitaka
 Divide the dough into any number you want

4.Wakati wa kusukuma tumia unga kuhakikisha unapata duara kubwa kiasi
  Sprinkle the plain flour onto the surface and roll the dough with rolling pin until you get bigger cycle

5.Yeyusha samli au blue band changanya na mafuta kupaka katika duara lako
  Mix the melted butter or ghee with cooking oil and brush on the top of the cycle

6.Kunja unavyopenda ila kumbuka jinsi unavyo ikunja ndio inatengeneza muonekano mzuri wa chapati
  Fold the chapati as you prefer but the chapati good looking depends on how you fold it

7.Baada ya kuziweka mafuta ni vizuri uziache kiasi cha dakika 10 mpaka 15 kabla ya kuzipika 
 After you fold them better to let them rest for atleast 10 to 15 minutes 

8.Sukuma chapati jitahidi upate duara zuri lenye shape ya kuvutia
  Roll the folded dough again to get a nice or perfect circular shape

9.Unapo sukuma chapati isiwe nyembamba wala nene sana iwe na upana wa kiasi
  Make sure it is neither too thin nor too thick

10.Chapati ikiwa nyembamba sana unapo ichoma huwa ina kakamaa na ikiwa nene sana huwa haiivi vizuri inaweza kuwa mbichi
 The thinner dough make chapati to be too crunchy after cooking and the thick chapati can result not to be cooked well inside 

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Moto hapa ndio kwenye mambo yote ukikosea chapati nayo inaweza kuwa mbaya
  Heat you use is very important,if you fail to set the required heat and the Chapati will not be good

2.Moto ukiwa mdogo hupelekea chapati kunyonya mafuta
 If you set minimum heat the chapati will absorb oil

3.Moto ukiwa mwingi chapati huungua
 If the heat is high the chapati will be burnt

4.Weka moto wa wastani ili uivishe chapati yako taratibu
 Make sure you set the medium heat during cooking

5.Weka chuma jikoni pakaa mafuta kijiko kimoja
 Heat the pan and add 1 Tbsp of Oil

6.Weka chapati yako jikoni
 Add the Chapati into the pan

7.Iache kidogo sana yaani ikisha kubadilika kutoka ubichi tu geuza upande wa pili
 Leave it for some second before it forms the bubbles flip it to the other side

8.Acha iive mpaka ianze kufanya rangi za kuiva
  Then let the other side cooked evenly till makes golden colour

9.Usiache mpaka ikaungua
 Don't let it burnt

10.Izungushe zungushe kwenye chuma ili sehemu zote zipate ile rangi ya kuiva hasa nchani mwa chapati
 Use your hand to circulate your chapati around the pan so as the corners will cook well

11.Ikunje sehemu mbili sawa
  Fold the Chapati in half

12.Weka mafuta kijiko kimoja
 Add 1 Tbsp of Oil

13.Penyeza kijiko kati kati ya chapati
  Insert the spoon in between of the folded chapati 

14.Fanya kama unaigandamiza huku ukiisugua na chuma
 Press it with spoon around the pan

15.Ongeza mafuta kidogo izungushe chapati hadi upate rangi nzuri ya kuvutia
 Add the little oil and circulate it to get beautiful colour

16.Geuza upande wa pili rudia hatua ya 13 mpaka 16
 Turn the other side of folded chapati and repeat step 13 until 16

17.Ikunjue irudi kuwa duara
 Unfolded the chapati to be in circular shape

18.Acha ule upande wa nyuma ya chapati uive kidogo tu
 Let the white layer to cook evenly

19.Itoe malizia kuchoma chapati zilobakia kwa hatua hizo ziliopo juu
 Remove from the pan and finish the remained chapatis by following above steps

20.Njia hii ya upishi wa chapati hupelekea chapati kuchambuka wakati wa kuipika chapati
 If you cook chapati by this way it makes chapati softer while it is still in a pan 

Angalizo:Note
1.Ukikosea kukanda unga na kuwa mgumu na hizi njia za chini zote zitakataa kutoa chapati laini
 Make sure you knead the dough till soft otherwise the chapati will not be soft

2.Ni vizuri kupika upishi huu ukiwa huna haraka taratibu kupata chapati nzuri
Do not hurry in  preparing and cooking chapati so as to get soft one

3.Ni upishi unaohitaji mazoezi pika mara kwa mara hadi utaziweza
  Make sure you cook chapati frequently so as to get used with it

Furahia Chapati Lainii.

12 comments:

Unknown alisema ...

Asante mumy

Unknown alisema ...

Karibu Riziki Bakar

Peter Felix alisema ...

Ninahitaji wapishi wazuri waliyesomea mapishi ya Vitafunwa, na vyakula mbalimbali kwaajili ya mgahawa wa kisasa. maombi yakiambatanishwa na vyeti yatumwe kwa anuani hii... peterluswema@gmail.com Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/8/2017.

Peter Felix alisema ...

Ninahitaji mpishi mzuri aliyesomea mapishi ya Keki na Mikate, maombi yakiambatanishwa na vyeti yatumwe kwa anuani hii... peterluswema@gmail.com Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/8/2017.

Unknown alisema ...

maji yapi yanafaa zaidi moto au baridi?

Unknown alisema ...

Asante mpenzi nimejua nilipokuwa nakosea mie huwa nazibebanisha hata tatu na huwa sikunji

Unknown alisema ...

Mahitaji hakuna vipimo hqkuna ni kukata tu donge limetokana na nn hakuna

Unknown alisema ...

Mwongozo mwema kweli asante

Unknown alisema ...

Asnt

Unknown alisema ...

Thanks for the clarification

Unknown alisema ...

Nimependa hii

Unknown alisema ...

Asante

Chapisha Maoni