Jumatano, 22 Juni 2016

KATLESI ZA MAYAI YA KUCHEMSHA(EGGS CUTLETS)




MAHITAJI
1.Viazi Mbatata Robo(1/4 kg)
2.Mafuta ya kula nusu lita
3.Mayai yaliyo chemshwa 6
4.Chumvi kiasi
5.Juisi ya Ndimu kijiko kikubwa 1
6.Pilipili ilosagwa Nusu kijiko cha chai
7.Mayai mabichi 3
8.Unga wa mchele au wa Sembe Vijiko vya Chakula 3
9.Maji kiasi


MAANDALIZI
1.Menya viazi mbatata kata vipande kiasi
2.Osha viazi weka maji na chumvi kiasi
3.Vunja mayai weka chumvi
4.Yapige mayai kisha weka pembeni
5.Menya mayai yalio chemshwa weka pembeni


JINSI YA KUPIKA
1.Chukua sufuria ulioweka mbatata acha ichemke mpaka viazi viwe laini na kuiva.
2.Kisha vimwage maji virudishe jikoni vikauke kwa dakika 1tu.
3.Epua viazi viponde kwa mwiko wa ugali mpaka vipondeke
4.Chukua viazi vilopondwa kiasi weka kwenye mkono tengeneza shimo la kuingia yai lilochemshwa
5.Weka yai kati kati ya shimo la viazi kisha weka sawa viazi kuficha lile yai
6.Rudia kwa mayai yote yalobakia
7.Nyunyizia unga kwenye maduara ya katlesi zako
8.Chukua karai mimina mafuta wacha yapate moto sana hadi yatoe moshi
9.Tumbukiza katlesi kwenye mayai mabichi kisha weka kwenye mafuta yamoto
10.Iache bila kuigusa kwa dakika 3 mpaka iwe ya brown
11.Igeuze kisha acha kwa dakika 3 nyengine toa chuja mafuta.
12.Inaweza kuliwa yenyewe au na chapati au mkate wowote



Angalizo:
1.Viazi usiviponde kama havijakauka vizuri vikiwa vya maji vitafanya maji ndani baada ya kuiva
2.Usiweke katlesi kama mafuta hayajapata moto vizuri
3.Hakikisha katlesi imezama kabisa kwenye mafuta la sivyo itapasuka kwenye karai
4.Unaweza kuweka bread crumbs ukikosa unga wa mchele
5.Usiweke unga wa ngano kama mbadala wa unga wa sembe
6.Mayai yachemshwe na chumvi kiasi



Furahia Katlesi Zako.


3 comments:

Unknown alisema ...

hii juici ya ndimu inatiwa wakati gani

Unknown alisema ...

somo zuri hata mm kesho wageni wangu nawaandalia kwenye break te#chefsaifary

Unknown alisema ...

Some zuri saana

Chapisha Maoni