Jumatatu, 21 Desemba 2015

VILEJA VYA ROUND(HOW TO MAKE PINWHEEL COOKIES)



MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Blue Band gram 300
   Blue Band 300 gram

2.Sukari gram 250
  Sugar 250 gram

3.Mayai2
  2 Eggs

4.Unga wa ngano 1Kg
  Flour 1Kilogram

5.Cocoa nusu kikombe
  Half cup of Cocoa powder

6.Arki Vanilla kijiko cha chai 2
  Vanillla Essence 2 Tablespoon

7.Arki ya Ice cream kijiko cha chai 1
  Ice cream Essence 1 Tablespoon

8.Baking powder kijiko cha chakula 1
  Baking powder  1 Tablespoon

9.Chumvi kiduchu
  A pinch of salt

10.Plastic wrap au mifuko meupe ya plastic 1
     Plastic wrap

MAANDALIZI/PREPARATION
1.Chekecha unga kisha uweke chumvi na baking powder na changanya vizuri
  Sift the flour added baking powder and Salt.

2.Saga blue band pamoja na sukari kwa mwiko wa ugali wa kwa hand mixer mpaka sukari ilainike vizuri kwa muda usiopungua robo saa
    Beat on medium speed until light and creamy. Gradually add the sugar and beat until fluffy

3.Vunja mayai na uyaweke huku ukiendelea kusaga kwa dakika 10
  Then add the eggs, one at a time, beating well after each addition

4.Weka arki zako zote mbili na uchanganye vizuri
   Then add the vanilla extract and ice cream essence and beat until well incorporated.
   
5.Weka unga wako kidogo kidogo mpaka uji wako uchanganyike na kuwa donge kubwa
   At low speed, gradually add the sifted dry ingredients.  Once the dry ingredients are added, increase speed to medium and beat until the dough leaves the sides of the bowl.

6.Ugawe sehemu mbili sawa moja weka cocoa mwengine uache kama ulivyo
  Devide the dough into 2 then one dough mix with cocoa and other kept aside.

7.Kisha gawa kila moja sehemu mbili yaani upate madonge meupe mawili na meusi hali kadhalika
   Shape both vanilla and chocolate dough into balls and slice each dough ball into two equal halves

8.Kisha sukuma donge jeupe umbo la pembe nne na sukuma jeusi pembe nne pia
   On a sheet of waxed paper, roll out half of the vanilla dough into a rectangle roughly 7 inches by 8 inches.  Do the same for one half of the chocolate dough.

9.Chukua plastic yako na weka donge jeusi ulilolisukuma kisha weka donge jeupe juu ya jeusi
 Flip the rolled vanilla dough onto the chocolate dough.

10.Kisha zungusha donge lako kwa msaada wa plastic likunje kama unakunja chapati kisha lifunge donge lako likiwa kwa hali ile ya urefu ukilizungushia plastic na weka kwenye friji kwa lisaa 1
    And then peel the waxed paper off of the chocolate dough.  Lightly press by gently running your rolling pin on the surface to remove any air pockets and ensure both are adhered .Starting with the short end facing you, tightly roll the dough into a log, and put in the fridge for atleast 1 hours

11.Rudia njia hizo kwa yale madonge mawili yaliobakia
   Repeat the same steps with the other half of the chocolate and vanilla dough so you get two cookie dough logs.

12.Toa kwenye friji na kata kata maduara madogo kiasi weka kwenye tray hakikisha kuna nafasi kati ya kileja na kileja
  Remove from refrigerator then roll each log on the counter to retain a round shape and prevent one side from flattening.When ready to bake, slightly thaw the dough just enough so you can easily slice it cleanly with a sharp knife. .Place on a cookie sheet lined with parchment paper allowing each cookie enough space to expand.

JINSI YA KUPIKA
1.Weka tray yako kwenye oven moto wa 100'C kwa muda wa dakika 10
   Put a tray in an Oven and bake for 100'C for 10 minutes

2.Kisha vigeuze juu chini rudisha tena jikoni
  Turn them upside down and return them in an Oven

3.Baada ya dakika 10 tayari vitakua vimeiva
  After another 10 minutes transfer the cookies onto a wire rack to cool.

4.Acha vipoe unaweza kula na kinywaji chochote
  Let them cool you can serve with any drinks

Angalizo:Note
1.Weka moto kulingana na jiko lako kama lina moto mkali uwe mara kwa mara unaviangalia
You can bake them according to your medium Oven Heat temperature

2.Usiviweke kwenye friji zaidi ya masaa mawili
Dont over refrigerate them

3.Unaweza kupikia mkaa ukipenda
 You can bake with charcoal(Mostly African)

4.Kama huna hand mixer usisage na blender
  If you dont have hand mixer dont blend the blue band mixture

Furahia Round Pinwheel Cookies Zako.

0 comments:

Chapisha Maoni