Ijumaa, 25 Desemba 2015

MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI)


MAHITAJI
1.Pakti ya Macaroni
2.Nyama ya kusaga robo
3.Kitunguu maji kidogo 1
4.Kitunguu thomu punje 3
5.Karoti kubwa kiasi 1
6.Pilipili boga 1
7.Nyanya(Tungule) kubwa 3
8.Mafuta robo kikombe
9.Chumvi kijiko cha chakula 1 na 1/2
10.Ndimu 1
11.Nyanya ya paketi robo
12.Royco pakti 1
13..Maji lita moja

MAANDALIZI
1.Osha Viungo vyote vinavyohitajika kuoshwa
2.Para keroti weka pembeni,kata kata kitunguu maji weka pembeni malizia kukata pilipili boga nyembamba weka pembeni
3.Twanga kitunguu thomu weka pembeni
4.Weka maji kidogo kwenye kibakuli kisha kamua ndimu yako vizuri
5.Saga nyanya zako ziache pembeni
6.Chukua nyama ya kusaga weka ndimu,chumvi na vitunguu thomu
7.Kisha tengeneza maduara ya nyama makubwa kiasi weka kwenye sufuria

JINSI YA KUPIKA
1.Yapange maduara ya nyama kwenye sufuria safi yafunike yaache yaivie mvuke na yabakie na maji maji kidogo
2.Pasua macaroni yako weka kwenye sufuria na maji na chumvi kisha yaweke jikoni yaache yaive mpaka yalainike kisha mwaga maji yaliobakia kwenye sufuria kwa kuyachuja macaroni yako
3.Rudisha sufuria jikoni acha ikauke maji na mimina mafuta
4.Yakipata moto kaanga vitunguu kisha pilipili boga na kisha karoti
5.Vikipiga brown weka nyanya na chumvi funika kwa dakika 3
6.Kisha ongeza nyanya ya paketi na royco
7.Mimina nyama ya kusaga acha kidogo
8.Sasa weka macaroni yale uliyo chemsha na koroga ili yachanganyike vizuri na nyama na viungo vyengine
9.Acha kwa dakika 2 rosti likipungua na kuingia kwenye macaroni vizuri epua mimina kwenye chombo chako cha kulia weka mezani
Angalizo:
1.Usiweke maji wakati wa kupika rosti hakikisha linakua zito zito
2.Pikia moto wa wastani upishi uwive taratibu
3.Hakikisha huunguzi vitunguu maji wakati wa kuvikaanga

Furahia Macaroni Yako.

0 comments:

Chapisha Maoni