Jumatatu, 21 Desemba 2015

MKATE WA SAMAKI(CHICKEN BREAD)


MAHITAJI
1.Unga wa ngano robo kilo
2.Samaki  vibua 3
3.Samli vijiko vya chakula 2
4.Ufuta robo kikombe
5.Yai 1
6.Chumvi vijikovya chakula 2
7.Karoti 1
8.Pilipili Boga(Pilipili hoho) 1
9.Pilipili Manga punje 10
10.Hamira vijiko vya chakula 2
11.Sukari kijiko cha chai 1
12.Maziwa ya unga vijiko vya chakula 2
13.Ndimu 1
14.Mdalasini wa unga kijiko cha chakula 1
15.Pilipili manga ya unga kijiko cha chakula kimoja
16.Uzile(binzari nyembamba) ya unga vijiko vya chakula 2
17.Royco kijiko cha chakula 1
18.Pilipili ya kuwasha 2
19.Kitunguu thomu punje 3
20.Maji nusu lita

MAANDALIZI
1.Chekecha unga kwenye chombo cha kukandia
2.Chukua kikombe kidogo weka maziwa ,hamira,sukari,chumvi na maji kiasi na mpaka iumuke
3.Ikiumuka iweke kwenye unga na changanya vizuri
4.Weka samli kijiko kimoja,vunja yai weka ute tu kiini kiweke pembeni kisha changanya tena unga wako
5.Weka maji taratibu mpaka ushikane na anza kuukanda
6.Kanda kwa dakika 10 na uache kwa dakika tano
7.Kanda tena mpaka ulainike kisha upake samli uache uumuke
8.Osha samaki vizuri muweke kwenye chombo cha kupikia
9.Mkamulie ndimu samaki wako,weka chumvi na royco
10.Osha Keroti na Pilipili boga kisha vikate kate na keroti uipare
11.Twanga pilipili na kitunguun thomu au saga weka pembeni

JINSI YA KUPIKA
1.Teleka samaki jikoni na maji kidogo sana mwache aive hadi abaki na vimaji kidogo
2.Mtoe miba yote ibaki nyama tupu weka kwenye bakuli
3.Weka viungo vya unga kwenye nyama ya samaki,keroti,pilipi boga na pilipili changanya vizuri
4.Onja nyama yako kama imekolea kila kitu weka pembeni kama bado utaongeza
5.Chukua unga uloumuka kata madonge upendayo idadi ya mikate utayopenda kutengeneza
6.Sukuma madonge uliyo yapata kwa urefu
7.Kisha chukua kisu kata nchani mwa donge lako ulilo lisukuma kwa urefu upande wa kulia na kushoto yaani liwe kama limechanwa chanwa
8.Kisha nenda hadi ncha ya juu pale kati kati kata pembe tatu ndogo sana  na ncha ya chini ukate pembe tatu kubwa
9.Weka mchanganyiko wako wa samaki kati kati na utandaze kwa urefu
10.Kisha chukua ncha moja moja ya kulia na kushoto fanya kama unasuka ulete kwa kati
11.Rudia njia hio mpaka umalize mkate wote upate umbo la samaki
12.Mpakae kiini cha yai samaki wako 
13.Mnyunyizie ufuta na mbandike pipilipili manga sehemu ya jicho
14.Muache aumuke kisha muweke kwenye oven
15.Mpika kwa moto wa 100'C mpaka awive
16.Acha apoe tayari kwa kula na juice au kinywaji chochote
Angalizo:
1.Kama huna haraka usiumue hamira kwa namna hio
2.Unaweza kutumia kuku,samaki au nyama kupika huo mkate
3.Kuwa makini na moto wasiungue

Furahia Mkate Wako.

0 comments:

Chapisha Maoni