Alhamisi, 28 Aprili 2016

WALI WA VIUNGO


MAHITAJI
1.Mchele wa Basmat Robo(1/4 kg)
2.Mafuta ya kula robo lita
3.Kitunguu maji kikubwa 1
4.Karoti kubwa 1
5.Pilipili Hoho(Pilipili boga) kubwa 1
6.Chumvi vijiko vikubwa 2
7.Uzile mzima(Binzari Nyembamba) kijiko kidogo 1
8.Mdalasini mzimakijiko kidogo 1
9.Hiliki punje 10
10.Giligilani nzima punje 15
11.Viazi Mbatata vidogo 8

MAANDALIZI
1.Osha mchele wako vizuri uweke pembeni
2.Katakata kitunguu maji,karoti na pilipili kila kimoja kata kwenye sehemu yake usivichanganye
3.Menya viazi mbatata kisha kata kata kwa umbola chipsi.


JINSI YA KUPIKA
1.Chukua sufuria weka maji na chumvi kijiko 1 yakichemka weka mchele wako acha uchemke na uive kidogo kisha umwage maji uache bila maji.
2.Chukua sufuria weka viungo vya pilau(Mdalasini,hiliki,giligilani na uzile) vikaange bila mafuta mpaka vitoe harufu epua viweke pembeni
3.Chukua sufuria nyengine uweke mafuta na kaanga chipsi mpaka ziive kisha zitoe
4.Ukitoa chipsi anza kukaanga vitunguu maji mpaka viwe brown kiasi kisha vitoe,halafu kaanga keroti na uzitoe na malizia kukaanga pilipili boga na kisha zitoe
5.Chukua chombo yatoe yale mafuta yote uliokaangia na bakisha sufuria tupu
6.Mimina wali uliopika kwenye ile sufuria kidogo kisha juu weka viazi mbatata,kisha ongeza wali kidogo juu ya viazi mbatata kisha weka pilipili boga ulilolikaanga kisha mimina wali juu weka vitunguu maji na rudia hivyo hivyo mpaka mwisho juu kabisa weka vile viungo vya pilau.
5.Nyunyizia chumvi kijiko kimoja juu ya wali wako
6.Mimina yale mafuta kidogo uliyo tumia kukaangia viungo vyako kisha ufunike wali wako upate kukauka
7.Acha wali ukauke kwa moto mdogo kwa dakika 5 usiukoroge.
8.Baada ya huo muda kupita uepue kisha uchanganye na upakue
9.Unaweza kula kwa rosti zito zito kama la maini,nyama au kuku

Angalizo:
1.Pangilia vizuri wali kwa kutenganisha na viungo vyako
2.Sio lazima upange kama nilivyo orodhesha hapo juu ila ni muhimu kutenganisha viungo na wali wako
3.Usiukoroge mpaka wakati wa kuupakua


Furahia Wali Wako.


0 comments:

Chapisha Maoni