Ijumaa, 22 Aprili 2016

CHAPATI ZA TUI LA NAZI


MAHITAJI
1.Unga wa ngano nusu kilo
2.Tui la nazi ml 500
3.Chumvi kijiko cha chakula 1na nusu
4.Sukari nusu kijiko cha chakula
5.Samli kikombe kidogo cha chai 1
6.Mafuta ya kupikia nusu kikombe

  
MAANDALIZI
1.Chunga unga wako weka kwenye chombo cha kukandia na punguza kikombe kimoja kidogo cha unga mkavu pembeni kwa ajili ya kusukumia
2.Weka chumvi,maziwa,sukari kisha changanya weka pembeni
3.Chukua tui,changanya taratibu mpaka ushikane na kuwa donge
4.Ukande kwa dakika 10 mpaka ulainike
5.Chukua bakuli lenye mfuniko weka donge lako la unga kisha pakaa donge lako lote samli kijiko cha chakula kimoja hakikisha samli inaenea vizuri
6.Funika unga wako kwa dakika 10 kisha utoe endelea kuukanda tena mpaka uwe unavutika kwa dakika 10
7.Katakata madonge kulingana na size ya chapati unayoitaka 
8..Sukuma madonge yako duara kwa kutumia unga mkavu kisha yapake samli kati na sokota na uyapange kwenye bakuli lenye mfuniko na uyaache kwa robo saa
9..Baada ya hapo utaanza kusukuma duara kwa ajili ya kupika chapati


JINSI YA KUPIKA
1.Yeyusha samli ilobaki changanya na mafuta 
2.Weka kikaangio chako jikoni hakikisha moto ni wa wastani
3.Weka chapati yako mpaka ifanye brown
4.Geuza Chapati yako upande wa pili ikiwa ya brown weka mafuta kijiko kimoja
5.Izungushe chapati yako huku ukiikandamiza na kijiko ili kuilainisha kati mpaka nchani 
6.Toa chapati weka nyengine mpaka umalize chapati zako
7.Unaweza kula yenyewe au na maharage,mchuzi,chai,juice,n.k.
8.Hizi chapati zinakuwa laini na ladha nzuri sana.
NB1.Ili chapati ziwe laini hakikisha unakanda kwa muda mrefu mpaka zinalainika
       2.Ipe mda wa kutulia kabla kuipika
       3.Usipende kuiweka mafuta mengi wakati wa kupika
       4.Usigeuze geuze mara kwa mara wakati wa kuchoma
       5.Fanya kama unaivunja vunja ikiwa ya moto kutoka jikoni 

Furahia Chapati Zako.

0 comments:

Chapisha Maoni