Jumatano, 26 Oktoba 2016

MAANDAZI YA KUOKA(MAANDAZI MAKAVU) BAKED ANDAZI




MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Unga wa ngano nusu
Flour 1/2 Kg

2.Sukari Kikombe cha Rice Cooker 1
  Sugar 1 Cup of Rice Cooker

3.Hiliki punje 10
 10 pieces Cardamon
 
4.Samli ya Aseel kijiko 1 cha chakula
  1 Tbsp Aseel Ghee

6.Tui la nazi glasi ndogo 1
  1 Glass Coconut Milk

7.Hamira Pakti 1
  1 Packet Yeast

MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Chekecha unga kwa kutumia chungio kwenye chombo utacho kandia unga wako kisha punguza unga nusu kikombe weka pembeni.
    In a big bowl sift flour and remove a half cup of it and set aside

2.Chukua kikombe kingine weka hamira,sukari kijiko 1,unga kijiko 1 na tui vijiko 3 iache kwa dakika 3 mpaka ifure.
  In an empty cup add yeast,1 Tbsp of sugar,1 Tbsp flour and 3 Tbsp coconut milk and let it rise

3.Twanga hiliki baada ya kuzimenya kisha weka kwenye unga unaotaka kuukanda
 Grind peeled cardamon and add them into the bowl having flour

4.Chukua unga ulio uweka hiliki,weka sukari na samli kisha changanya kwa mkono vizuri.
   Add ghee and sugar into the flour and mix it well with your hand

5.Chukua hamira ilio umuka changanya kwa mkono vizuri na unga wako 
    Add raised ghee into the flour mixture and keep mixing 

6.Malizia kwa kumimina tui lako kidogo kidogo na uanze kuukanda utakapo kuwa donge moja.
    Finally pour coconut milk little by little into the flour mixture until you get a dough

7.Kanda unga kwa dakika 10 mpaka uwe mlaini kisha ufunike vizuri au uweke kwenye container na uufunike ili usipitishe hewa uache kwa dakika 5 kwenye sehemu ya joto.
   Knead the dough at least for 10 minutes until soft then cover it for 5minutes let it rise in double size 

8.Ukiumuka kata madonge na uyasukume kwa kutumia unga mkavu upate duara ila lisiwe nene sana wala jembamba sana,kisha kata maandazi yako kwa shape ya pembe tatu.
 Than cut into medium dough and roll it out to get a circle after sprinkle the flour on to the surface,then cut the circle into four rectangular pieces(maandazi) 

9.Weka unga mkavu kwenye tray na ueneze kisha panga maandazi unayotaka kuoka 
 Sprinkle the remained flour on the tray and add the maandazi into the tray
   
10.Yaache maandazi yako yaumuke kwa dakika zisizo pungua 20.
    Let them rise for 20 minutes

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Washa Oven Moto wa juu na chini 140'C
  Heat the oven 140'C(Upper and Lower Heat) 

2.Pika Maandazi yako kwa muda wa dakika 20 tu
   Bake them for 20 minutes only

3.Yakianza Kupiga rangi ya dhahabu yatoe kama yanavyoonekana kwenye picha ya chini
    When turn into golden colour remove them into the oven as seen in the picture below

4.Acha yapoe kidogo toa weka kwenye sahani
   Let them cool and take them into the plate

5.Tayari kwa kula na Maharage,mboga,mchuzi,chai au kinywaji chochote 
    Ready to serve with Cooked Beans,Source,Tea or any other drinks



                    



Angalizo:Note
1.Hakikisha unga unaukanda vizuri hadi unakuwa mlaini ili maandazi yawe laini pia
   Make sure the dough is too soft to have soft andazi

2.Kama maandazi mengi hifadhi kwenye kontena ili mpaka siku ya pili yawe malaini
   You can keep cooked maandazi into tight container to remain soft for more than one day

3.Hakikisha yanaumuka vizuri kabla ya kuyaoka
   Let them rise well enough before baking them

4.Unaweza kuoka kwenye mkaa pia kama huna oven
   You can also bake them by using coal stove

5.Unaweza Kutumia samli yoyote kama huna ya Aseel au tumia siagi ukikosa samli
   You can use any type of ghee or butter instead of Aseel Ghee

6.Fuata maelezo na vipimo vizuri ili kupata maandazi mazuri kama yanavyoonekana kwenye picha
   Make sure you follow the exactly measurement,ingredients and instructions to get nice Andazi

Furahia Maandazi Makavu.

4 comments:

Unknown alisema ...

Kwa kuwa unalenga kimataifa, nikupe marekebisho machache muhimu
1 pembetatu ni triangle, sio rectangle.
2.mchuzi ni sauce, sio source
3.the blog is written in English ..... sio by english...

���������������� ������������ alisema ...

Je unaezapika kwa kutumia gas???

���������������� ������������ alisema ...

Kibua

Unknown alisema ...

i like it napika leo😅

Chapisha Maoni