Alhamisi, 21 Julai 2016

SAMBUSA ZA KUBABUA ZA NYAMA (MINCEAD MEAT SAMOSA)


1.Nyama ya kusaga robo
 1/4kg Minced Beef

2.Vitunguu maji vikubwa kiasi 3
  3 medium size Onion

3.Vitunguu thomu vilotwangwa kijiko cha chai 1
  1 Tea spoon  Garlic Cloves 

4.Tangawizi Vijiko vya chai 2(ilotwanga)
 2 Tea spoon minced Ginger

5.Pilipili ya kuwasha ilotwangwa kijiko cha chai 1(au zaidi kama mpenzi wa pilipili)
 1 Tea spoon Chili(Chopped or crushed)or more if you like chilli

6. Chumvi kiasi
 Salt to taste

7.Maji kiasi
  Some Water

8.Mdalasini wa unga nusu Vijiko vya chakula 2
   2 Tbsp Cinnamon powder

9.Uzile(Binzari nyembamba) ya unga Vijiko cha chakula 2 
    2  Tbsp Cumin powder

10.Mafuta ya kusukumia Kikombe kidogo cha chai
    1 Cup Cooking Oil

11. Mafuta ya kupikia lita 1  
       1 Litre of Cooking Oil

12.Pilipili hoho(Pilipili boga) ndogo 1(Ukipenda)
 1 Green pepper (Optional)

13.Karoti ndogo 1(ilioparwa) (Ukipenda)
 Grated carrots (Optional)

14.Njegere robo kikombe (Ukipenda)
 ¼ Cup Green Peas(Optional)

15.Uji wa Unga wa Ngano robo kikombe
¼ Cup Heavy wet mixture of plain flour and water

16.Unga wa Ngano Nusu
 1/2 Kg Plain Flour


MAANDALIZI/PREPARATION
1.Changanya kitunguu thomu,pilipili,tangawizi na uviweke pembeni
   Mix red chilli,ginger and clove of garlic in a bowl and keep it aside

2.Menya kitunguu maji,karoti
 Peel the onion and carrots

3.Kisha kata kitunguu maji vidogo vidogo katika umbo la pembe nne
 Chop the onion into small qubes

4.Katakata Pilipili hoho ndogo ndogo
 Chop the Green Pepperinto small pieces 

5..Andaa bakuli jengine weka unga wa ngano na chumvi kiasi kisha uchanganye vizuri 
 Into separate bowl mix plain flour and salt

6.Weka maji taratibu  kwenye bakuli la unga mpaka ushikane
  Add little water till you get the dough

7.Kanda unga kidogo tu usiwe mlaini
  Knead the dough for some minute make sure the dough is not soft

8.Gawa donge lako katika maduara matano tano
  Divide the dough into 5 small balls

9.Kisha yakatamize kwa mkono upate vichapati viduchu vitano
 Press your balls by hand to get small cycle

10.Chukua mafuta kwenye kikombe mimina juu ya kichapati kimoja kama vijiko vitatu.
 Add two table spoon of oil on top of the cycle

11.Weka donge jengine juu ya lile la kwanza halafu mimina mafuta kama ulivyofanya mwanzo
 Take another cycle keep on top of the first cycle and pour some oil as you did before

12.Rudia kuweka madonge juu ya nyengine mpaka umalize yote matano
  Repeat the above process till you finish all five dough

13.Chukua kifimbo Sukuma madonge yote kwa pamoja mpaka upate lichapati kubwa
  Use a rolling pin to flatten all five dough together to get a big cycle


JINSI YA KUPIKA
1.Weka nyama jikoni tia chumvi, usiweke maji acha itoe maji yenyewe hadi iwive
  In a medium heat cook the minced beef add salt only and let it dry

2.Ikiiva epua nyama acha ipoe
  When it’s ready remove from the stove and let it cool

3.Changanya nyama yako vizuri weka mchanganyiko wa tangawizi,mdalasini,uzile na uichanganye vizuri
 Then add mixture of ginger,cinnamon powder,cumin powder in the cooked minced beef 

4.Weka kitunguu maji,karoti,pilipili hoho,njegere ulivyovikata weka kwenye nyama
 Add Chopped Onion,Carrot,Green Pepper,green peas in the minced meat

5.Kisha changanya vizuri na uonje
  Keep mixing the meat mixture and taste it


6.Kama iko sawa endelea
  If it is okay proceed to the next step

7.Chukua lile lichapati liweke kwenye chuma cha kupikia chapatti kwa moto mdogo kiasi
 In a medium heat add the flatten dough into the pan

8.Ikiianza kufanya vibofu na rangi ya dhahabu kwa mbali ligeuza
  Turn to the next side so can be cooked evenly when turn into light golden colour

9. Upande wa pili ukibadilika rangi utoe
  Take out from the pan when the other side is done

10.Chukua kisu ikate upesi upesi pande nne zenye umbo la pembe tatu
 Take a nife or pizza knife slice to get four triangle



11.Ikiwa ya moto ibandue haraka haraka kila pembe tatu utoe pembe tano kwa kila pembe tatu moja
  While it is hot take each triangle unbind it to get five triangle to each one

12.Hakikisha unapata jumla ya papi(manda) 20 za umbo la pembe tatu
  Make sure you got 20 triangular pastry as a total of four pastry

13.Chukua papi(manda) moja kutanisha pembe mbili kisha weka nyama kati kati
    Take one pastry ,make sure the two end meet at the center then add the meat minced inside of it

14.Chukua uji wa unga wa ngano pakaza katika ile ncha moja ilobaki kwa ndani na ibane mpaka ile ncha ifike kati kati
 Take the wet flour mixture apply in the inner side of the third end then bind by keeping it to the center of the pastry

13.Rudia mpaka umalize sambusa zote
   Repeat the procedure till you finish all samosa

14.Weka mafuta kwenye karai
    Add the Cooking Oil into the frying pan 

15.Mafuta yaache yapate moto kiasi
   Bring the pan to the medium heat 

16.Weka sambusa zako kulingana na ukubwa wa karai
   Add the samosa according to the size of your frying pan

17.Ziache dakika kadhaa zikiwa za rangi ya dhahabu ilokoza zigeuze na ziwache kidogo
   Leave for some minutes and turn into other side when it changes to golden colour 

13.Zikiwa za kote zitoe weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta
  When they turn into golden brown completely take them out from the pan into sieve or tissue

14.Zikipoa unaweza kula zenyewe au najuisi au mkate
  When they are slightly cool You can serve with bread,chapati,juice or as they are. 

Angalizo:Note;
1.Ili sambusa ziwe nzuri hakikisha zinachapuka viungo vizuri
        Marinate the minced meat mixture well to get samosa with good taste

      2.Sukuma ukubwa wa chapatti kulingana na chuma chako cha chapatti
        Flatten dough size should exceed the size of your pan

      3.Wakati wa kuzipika hakikisha mafuta yasiwe na moto sana
          Don’t heat the oil to the maximum

      4.Zipike taratibu usizifanyie haraka kuzigeuza hakikisha zinapiga rangi ya dhahabu ndio uzigeuze
        Don’t turn into other side if the other side is undone  

    5.Wakati wa kusukuma yale madonge matano usisukumie unga hata kidogo yale mafuta yanatosha
 When you roll out to flatten the dough don’t add or sprinkle the plain flour on top of the dough


Furahia Sambusa Zako


3 comments:

Ashura Ramadhani alisema ...

Nashukuru kwa kunifundisha kupika sambusa nitajaribu nyumbani na mimi kuzipika.

Unknown alisema ...

Usijali Dear Ashura Ramadhani Ukipika usisahau kuniletea nionje

Unknown alisema ...

nimejifunza ahsante sana

Chapisha Maoni