1.Maharage 1/4 Kg
1/4 Kg Fresh Beans
2.Tui Jepesi Kikombe Kikubwa 1
1 Mug Light Coconut Milk
3.Tui Zito 1/4 Kikombe
1/4 Mug Heavy Coconut Milk
4.Kitunguu thomu Kilotwangwa kijiko cha chai 1
1 Tea spoon Mashed garlic
5.Kitunguu maji kilokatwa 1
1 Sliced Onion
6.Pilipili boga ilokatwa 1
1 Sliced Green pepper
7.Kerot Iloparwa 1
1 Grated Carrot
8.Chumvi kijiko cha chakula 1
1 Tbsp Salt
9.Mafuta ya Kula vijiko 2
2 Tbsp Cooking Oil
10.Royco Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Royco
11.Nyanya zilizo sagwa 3
3 Blended Tomato
12.Maji ya kuchemshia Kiasi
Water for Boiling
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Safisha maharage ondoa uchafu wote na yaoshe vizuri
Remove all unwanted particle in beans then wash them well
2.Weka kwenye sufuria kisha yaweke maji
Add them into cooking pot and pour some water
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Funika sufuria kisha chemsha maharage mpaka maji yapungue
Cover the pot and bring them to boil till the water level decrease
2.Ongeza maji mengine yaache yachemke mpaka yapungue
Pour some water and let them boil till the water level falls down
3.Sasa weka maji kidogo kidogo yasifunike maharage yako ili yaive bila ya kutoka magamba
Add some little water make sure the water level do not cover the beans
4.Endelea kuongeza maji kidogo kidogo mpaka yaive
Keep adding some water until cooked
5.Katika sufuria nyengine weka mafuta acha yapate moto
In another pot add oil and let it heat for a minute
6.Weka vitunguu maji vikaange hakikisha haviungui
Add onion and fry them till brown make sure they are not get burnt
7.Ongeza Pilipili boga na ikaange vizuri
Add green pepper and keep frying
8.Weka Kerot endelea kukaanga
Add grated carrots and keep frying
10.Mwisho weka kitunguu thomu na endelea kukaanga
Lastly add garlic and keep frying
11.Mimina nyanya zilizo sagwa kisha koroga mchanganyiko wako
Pour the blended tomato and stir your mixture
12.Weka chumvi na royco kisha funika acha ichemke kwa dakika 1
Add salt and royco and let it boil for 1 minute
13.Mimina maharage yaache kwa dakika 1
Add cooked beans and let it boil for 1 minute
14.Kisha mimina tui jepesi acha lichemke kwa dakika 3
Pour light coconut milk and let it boil for 3 minutes
15.Mimina tui zito kisha yakoroge maharage yako kidogo acha lichemke kwa dakika 2
Pour heavy coconut milk and stir the mixture and let it boil for 2 minutes
16.Epua acha kiasi cha dakika 5 ndio uyapakue
Remove from the heat and let them cool for atleast 5 minutes before serve
17.Unaweza kula na wali,ugali au mikate
You can serve with rice,ugali or bread.
Angalizo:
1.Hakikisha maharage yanaiva vizuri kabla ya kuyapika na bila kubanduka maganda
Make sure the beans are boiled well without removing its cover before frying them
2.Ili maharage yawe mazito hakikiksha yanapoa kidogo ndio uyapakue
In order to get heavy sauce let them cool before serve them
Furahia Maharage Yako
0 comments:
Chapisha Maoni