MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Siagi Robo kilo(1/4 Kg)
1/4Kg Butter
2.Sukari Robo kilo(1/4 Kg)
1/4 Kg Sugar
3.Unga Robo kilo(1/4 Kg)
1/4 Kg Plain Purpose
Flour
4.Mayai 6
6 Eggs
5.Arki Vanilla Kijiko cha chai 1
1 Tea Spoon Vanilla
Essence
6.Cocoa Vijiko vya Chakula 3
3 Tbsp Cocoa Powder
7.Baking Powder Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Baking Powder
8.Chungwa 1
1 Orange
7.Maganda ya Chungwa Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Orange Zest
8.Chumvi Kiduchu
Pinch of Salt
9.Fruit Cake Kikombe Cha Chai Nusu(Sio Lazima)
1/2 Cup Fruit Cake(Optional)
10.Juisi ya Chungwa Vijiko 3
3 Tbsp Lemon Juice
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Chekecha unga kwenye bakuli kisha weka chumvi na baking
powder na uchanganye vizuri kwa mwiko
In a bowl sift the
flour then add baking powder and salt,mix them very well by using spartula
2.Osha chungwa vizuri kasha lipare kwa kipario ili upate
maganda yake kijiko kimoja
Wash an orange then
grate it till you get one spoon of its zest
3.Weka maganda ya chungwa na Fruit Cake kwenye ungana
uchanganye tena vizuri
Add the orange zest
and Fruit Cake in a bowl of flour and mix them very well
4.Weka sukari na siagi kwenye bakuli jengine
In a separate bowl
add sugar and butter
5.Saga mchanganyiko wako kiasi cha dakika 3
Beat the mixture for
atleast 3 minutes
6.Weka Vanilla endelea kusaga kiasi cha dakika 2
Then add vanilla and
keep beating the mixture for 2 minutes
7.Weka mayai yako moja moja mpaka yamalize huku ukiendelea
kusaga
Add the eggs one by one
until you complete them alland keep beating the mixture
8.Weka juice ya chungwa kisha saga tena kidogo
Add lemon juice and
keep beating the mixture
9.Malizia kuweka unga kidogo kidogo mpaka umalize wotehuku
ukisaga
Lastly add flour
little by little till it finish and beat your mixture
10.Chukua bakuli chota mchanganyiko wako weka miko 3
In a small bowl add
your butter mixture atleast 3 spatula of it
11.Kisha weka cocoa kwenye kibakuli uloweka mchanganyiko
wako changanya vizuri kwa kijiko kikubwa
Add cocoa in that
mixture and mix it well by using table spoon
12.Washa Jiko la Umeme moto wa nyuzi joto 160
Pre heat the oven
160’C
13.Chukua trei weka karatasi ya kupikia
In a tray add baking
paper
14.Kisha Anza kuweka mchanganyiko mweupe na kati weka wa
cocoa kasha malizia mweupe
Start to add white
butter mixture and the cocoa mixture at the middle and the white mixture on top
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka trei jikoni kwa muda wa dakika 50 ndio fungua jiko na
tizama keki yako
Bake the cake for 50
minutes then open the oven to check it
2.Ingiza kijiti kisafi kwenye sehemu mbali mbali za keki
yako kuangalia kama imeiva
Insert the tooth pick
in the cake to check if it is cooked well and done
3.Ikiwa kijiti kitatoka na umaji maji basi keki yako bado
rudisha jikoni
If the tooth pick
seems to be wet the cake its not yet cooked return it in the oven
4.Kijiti kikitoka kikavu zima jiko toa keki wacha ipoe
If the spoon comes
dry switch off the oven and remove the cake let it cool
5.Ikipoa toa kwenye trei na ikate vipande tayari kuliwa na
kinywaji upendacho
When it is cool cut
it into pieces and serve with any drink you prefer
Angalizo:Note;
1.Hakikisha unafata vipimo sahihi vya
unga,siagi,sukari,baking powder na mayai ili upate keki nzuri
Make sure you use appropriate
measurement of butter,sugar,plain purpose flour,baking powder and eggs for best
result of the cake
2.Ukikosea vipimo vya keki hupelekea kutoiva au kuwa ngumu
When the cake
ingeredients are misused may not give you soft cake or it may not cooked evenly
3.Kuwa makini na jiko lako kama lina moto mkali tumia nyuzi
joto ambazo hazitounguza keki yako
You know well your
Oven so make sure you set appropriate Degrees that may not burn the cake
4.Tumia Chombo ambacho mchanganyiko wa keki hautojaa mpaka
juu ili ipate nafasi ya kuiva vizuri kwani ikipata joto hufura na huweza
kupelekea mchanganyiko ukamwagika kabla ya kuiva
Use the tray that has
enough space that may not lead the cake mixture to rise and comes out when it
is heated
5.Unaweza kupika kwa kutumia mkaa pia
You can even bake by
using charcoal
6.Hakikisha hukati keki yako mpaka ipoe inaweza kupelekea
kukatika katika
Make sure you do not
cut your cake if it is not cool enough
7.Keki inaweza kukaa mpaka siku 3 mpaka 4 kwenye mazingira
ya joto na siku 6 mpaka 7 kwenye mazingira ya baridi bila kuharibika
The cake can stay up
to 3 to 4 days in hot areas and 6 to 7 days in cold areas
Furahia Keki Yako.
0 comments:
Chapisha Maoni