MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Mchele wa Basmat Kilo
1 Kg Basmat Rice
2.Nyama ya Ngombe Kilo 1 na Nusu(Stake)
1 1/2 Kg Cow Fillet
3.Vitunguu Maji Nusu Kilo
1/2 Kg Onion
4.Vitunguu thomu Vijiko vya Chakula 2
2 Tbsp Mashed Garlic Cloves
5.Tangawizi Kijiko cha chakula 1
1 Tbsp Mashed Ginger
6.Chumvi kiasi
Salt To Taste
7.Mafuta Ya Kupikia Lita 1
1 Litre Cooking Oil
8.Viazi Mbatata Vikubwa Kidogo Nusu
1/2 Kg Potatoes(Medium in size)
9.Mtindi Glasi 1
1 Glass Yogurt
10.Kotmiri Fungu 1
1 Batch Coriander
11.Nyanya za Mchuzi(Tungule) kubwa kidogo 10
10 Medium size Tomato
12.Nyanya ya Paket (Tomato Paste)2
2 Packet Tomato Paste
13.Rangi ya Zafarani(Orange) kijiko cha chai 1
1 Tea Spoon Saffron
14.Rangi Nyekundu ya Unga Kiduchu
A pinch of Red colour(powder)
15.Zabibu Nusu Kikombe
1/2 Cup Raisin
16.Biriani Masala Kiasi
Some spoons of Biriani Masala
17.Kerot kubwa 1
1 Large Carrot
18.Pilipili Boga kubwa 1
1 Large Green Pepper
19.Sukari Kiduchu
A pinch of Sugar
20.Maji kiasi
Some water
21.Njegere Kikombe Cha Chai 1(Ukipenda)
1 Cup Green Peas
22.Ndimu iliokamuliwa 1
1 Lemon Squeezed
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Menya Vitunguu Maji na uvioshe
Peel the Onion and rinse them
2.Kata kata vitunguu maji kwa umbo la duara weka pembeni
Chop the onion in circular shape and keep them aside
3.Menya Viazi Mbata ,vioshe na weka pembeni
Peel the Potatoes rinse them and keep in the bowl
4.Osha kotmiri hakikisha haibaki na michanga
Rinse the coriander well to remove all dirty particles in it
5.Osha nyanya zikate kate weka kwenye jug la blenda pamoja na kotmiri kisha zisage
Rinse the tomato,chop them and blend them with coriander
6.Para kerot weka pembeni
Grate the carrots keep aside
7.Kata kata pilipili boga weka pembeni
Chop the Green Pepper
8.Chukua kikombe weka rangi ya zafarani na maji kiduchu kisha ikoroge
In a cup add saffron add some drops of water and mix it
9.Weka rangi ulioiweka maji kwenye viazi mbatata usiiweke yote ibakishe
Put some drops of saffron colour not all of it in the peeled potatoes
10.Zichanganye vizuri mbatata ili zienee rangi
Flip the potatoes to make sure they are covered well with orange colour
11.Kata kata nyama ioshe weka kwenye sufuria
Chop the fillet into medium pieces
12.Osha mchele vizuri mwaga maji acha kwenye bakuli
Rinse well the basmat rice and drain it
13.Chukua kikombe kingine weka rangi nyekundu na maji kiduchu
In a separate cup add red colour add some drops of water and mix it
JINSI YA KUPIKA/HOWTO COOK
1.Katika sufuria yenye nyama weka chumvi kiasi,tangawizi na vitunguu thomu kijiko kimoja
In a pan add chopped fillet ,salt,ginger and 1 table spoon of garlic
2.Chemsha nyama hadi iive
Bring it to boil till cooked well
3.Weka sufuria nyengine weka maji na chumvi acha yachemke
In a separate bowl add some water and salt let it boil
4.Yakiwa tayari mimina mchele na njegere acha viive kidogo mchele usiive kabisa kabisa uwe na kiini
When water comes to boil add rice,green peas let them cooked,but the basmat rice should not cooked till soft
5.Ukiwa tayari umwage maji uache kwenye chujio
Drain it and leave it to the colander
6.Weka mafuta kwenye karai acha yapate moto
Pour some oil in a frying pan
7.Kisha kaanga Vitunguu maji mpaka viwe rangi ya dhahabu hakikisha haviungui
Add the chopped onion and fry them until golden brown
8.Vikiiva vitoe acha vichuje mafuta
When they are done remove from the pan to the colander
9.Weka Viazi mbatata kwenye karai vipike hadi viwe rangi ya dhahabu bia
Add potatoes and fry them until golden brown
10.Vikiiva toa na mimina mafuta pembeni bakisha mafuta kidogo kwa ajili ya kukaangia
Remove from the frying pan to the colander(sieve),take some spoons of oil you used for frying potatoes into cooking pot
11.Kisha weka vitunguu thomu vilivyobakia kaanga kidogo
Add 1 table spoon of garlic remained into the pot having oil and fry it
12.Mimina Nyanya iliosagwa na kotmiri
Pour the mixture of blended tomato into the pot and keep frying for some seconds
13.Weka chumvi kiasi kisha weka viazi mbatata
Add salt then add potatoes
14.Funika acha vichemke kwa dakika 1 kisha weka nyama
Cover the pot for 1 minutes then add boiled fillet
15.Koroga kidogo kisha weka Nyanya ya paket na sukari
Use a spatula to stir the mixture then add tomato paste
16.Koroga vizuri na uache kidogo kisha weka Biriani Masala
Keep stirring well then add Biriani Masala
17.Koroga kisha onja na weka ndimu
Add lemon juice and keep stirring the mixture
18.Mimina mtindi acha kwa dakika 1 uchemke
Pour yogurt and leave for a minute let it boil
19.Malizia kuweka vitunguu maji viliokaangwa
Finally add the fried onion in the mixture
20.Koroga ukiona unakuwa mzito epua weka pembeni
Keep stirring leave for some second when it started to be heavy sauce remove from the stove
21.Chukua sufuria nyengine kubwa kiasi mimina lile rosti
Take large cooking pot pour the sauce
22.Kisha juu yake mimina wali na zabibu
Add rice and raisin on top of the source
21.Juu ya wali nyunyizia rangi ya zafarani iliobaki
On top of rice add some drops of remained saffron
22.Kisha Nyunyizia rangi nyekundu
Then add the drops of red colour on top of rice
23.Malizia kwa kunyunyizia mafuta kidogo juu ya wali
Lastly pour some drops of oil on top of rice
24.Ufunike weka mkaa wa moto juu ya wali ukauke vizuri na chini moto mdogo mdogo
Cover the pot and some charcoal on top.If you don't have put the pan into the oven so can be cook evenly
24.Baada ya dakika kadhaa Biriani lipo tayari
After some minutes the Biriani is ready
25.Chukua bakuli kubwa Anza kutoa wali wote kisha uchanganye kwa kutumia mwiko
Take big bowl with spatula then remove the all rice from the pot
26.Kisha changanya rosti lako vizuri
Then stir the sauce remained into the pot
27.Chukua Sahani Pakua wali kisha rosti juu Biriani tayari kuliwa
Take a spatula and add rice into the plate and sauce on top of rice
28.Unaweza Kula na Kinywaji Upendacho
You can serve with a drinks of your choice
Angalizo:Note;
1.Lazima utumie Mchele wa Basmati ili kupata Ladha na Muonekano mzuri
You must Use Basmat Rice for better result and taste
2.Ukichemsha Mchele hadi ukaiva biriani lako halitonyooka mchele utakuwa bwabwa
Do not over boil the Basmat rice
3.Mafuta ya vitunguu yakiwa hayajapata moto vizuri vitunguu vitanyonya mafuta
Do not add onions if the oil is not heated well
4.Vitunguu Vikiungua Biriani litakuwa chungu
Do not burn the onion it will result the sauce to have bitter taste
5.Ukiweka moto wa chini mwingi wakati wa kulikausha biriani rosti litakauka na mchuzi kuwa mdogo
Make sure the lower heat is not high it will dry the sauce in the oven
6.Usikaushe wali sana unakuwa mkavu wakati wa kuupakua
Do not dry the rice for a long time into the oven when its ready remove it
7.Usiweke mafuta mengi wakati wa kukaanga mchuzi na juu ya wali hupelekea chakula kuwa na mafuta mengi sana
Do not add too much oil it during frying and on top of rice.
8.Kama hupendi pilipili usiweke Biriani Masala nyingi
Do not add too much Biriani Masala the food will be too chilli
The served Biriani in the plate
Furahia Biriani Lako.
0 comments:
Chapisha Maoni