Urojo ni mchanganyiko wa vyakula mbali mbali pamoja na uji uji wake katika bakuli moja.
Hapa nitaeleza jinsi ya kuupika huo uji(urojo) mpaka kukamilika kwake.
Asili ya urojo ni India ila kwa sasa nchi mbali mbali zina andaa upishi huu.
Na Zanzibar ni mlo unaopendwa na maarufu sana.Na hii ndio aina ya urojo unaopikwa Zanzibar.
Zanzibar Mix(Urojo) is the dessert prepared by mixing different foods(dessert) with sauce in a bowl.
Its origin is India but now many countries prepared by there own style.
Also in Zanzibar we have our own style on how to prepare Urojo.
I can help you on how to cook this dessert so follow my recipe as follow
Kwenye Urojo Tunaweka/Things added in Mix(Urojo)
Boiled Potatoes
2.Mayai Ya Kuchemsha(Ukipenda)
Boiled Eggs(Optional)
3.Badia
Badia
4.Chatne
Chatne
5.Chipsi Za Muhogo
Cassava Chips
6.Mishkaki
Barbeque
7.Kachori
Kachori
7.Katlesi(Ukipenda)
Cutlets(Optional)
8.Na urojo wenyewe
Urojo Sauce
9.Pilipili(Ukipenda)
Chilli Sauce(Optional)
Baadhi ya vitu hapo juu nimeshavielezea kwenye blog yangu kwa hio nitaweka links za jinsi ya kuvipika hivyo vitu hapa nitaelezea jinsi ya kupika urojo tu
HIZI NI LINKS ZAKE
Badia na Chatne(Badia and Chatne) http://mapishiclassic.blogspot.com/2015/11/badia-za-kunde-na-chatne.html
Kachori http://mapishiclassic.blogspot.com/2016/08/kachori.html
Katlesi(Cutlets) http://mapishiclassic.blogspot.com/2015/11/mahitaji-1.html
Mishkaki(Meat Barbeque) http://mapishiclassic.blogspot.com/2015/12/mishkakibarbeque.html
Chipsi Za Muhogo(Fried Cassava Chips) http://mapishiclassic.blogspot.com/2016/02/chipsi-za-muhogocassava-chips.html
Some of the dessert added in urojo have already explained in my blog on how to prepare them. So I will just keep the links on how to get those recipe.Here I will explain only on how to cook Urojo.
HERE ARE THE LINKS
MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Unga wa Ngano Mug 1
1 Mug Plain Flour
2.Ndimu zilokamuliwa 2
Lemon Juice(2 Lemon)
3.Maji Lita 2
2 Litre Water
4.Chumvi Kiasi
Salt to taste
5.Bizari Kijiko cha chai 1
1 Tea spoon Turmeric Powder
MAANDALIZI/PREPARATION
1.Weka unga kwenye bakuli kisha weka maji nusu lita pamoja na bizari
In a bowl add flour,turmeric powder and half liter of water
2.Koroga hadi uhakikishe mabonge yote yameisha
Stir the mixture until well combined
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Mimina maji Yalobakia kwenye sufuria weka chumvi kiasi acha yachemke sana
Pour the remaining water in the pot with salt and let it boil
2.Kisha mimina uji wenye bizari kwenye maji ya moto taratibu huku ukikoroga mpaka uchanganyike
Add the turmeric mixture in the boiled and stir it throughly
3.Acha uchemke kidogo kisha mimina ndimu yako na ukoroge kidogo
Let it boil for a minute than add the lemon juice and stir the mixture
4.Acha uchemke onja chumvi na ndimu kama zipo sawa epua
Let it boil for some minutes than taste the salt if its okay remove from the heat
5.Ikiwa urojo ni mzito sana ongeza maji acha uchemke kidogo kisha uepue
If urojo sauce is very heavy add some water to lighten it
Angalizo:
1.Kama urojo ukiwa mkali au una chumvi nyingi ongeza maji kidogo kidogo mpaka upungue ukali
Add little water in the sauce if it salty or sour before you remove it from the heat
2.Hakikisha huuachi jikoni kwa muda mrefu mpaka ukaungua
Make sure you do not let it burnt
3.Usiweke maji mengi ukawa mwepesi kupitiliza
Do not add too much water the sauce will be too light
Jinsi ya Kuuandaa/How to serve it
1.Menya Viazi Mbatata ulivyovichemsha kisha vipasue kati na vikate vipande vidogo vidogo
Take a boiled potatoes and peeled them and cut them into small pieces
2.Menya Mayai yaliochemshwa na yapasue kati na kata vipande vinne
Peel the boilede eggs and slice into 4 pieces
3.Chukua Bakuli na kijiko
Take a bowl and spoon
4.Weka vipande vya viazi ulivyovikata katika kibakuli chenye kijiko
Add some pieces of boiled potatoes in a bowl having spoon
5.Weka na vipande vya mayai kwenye bakuli
Add pieces of eggs
6.Malizia kuweka kachori,badia,mishkaki,chipsi za muhogo na katlesi
Then add badia,kachori,barbeque,cassava chips and cutlets
7.Kisha mimina urojo kiasi upendacho
After that pour the urojo sauce in the bowl
8.Weka chatne na pilipili
Lastly add chatne and chilli sauce
9.Upo tayari kuliwa wenyewe au na mkate upendao na kinywaji upendacho
Ready to serve with bread,any drinks or as it is
Bakuli lenye urojo kama linavyoonekana
The bowl having Mix(Urojo) as seen after served
Furahia Urojo Wako
0 comments:
Chapisha Maoni