Alhamisi, 3 Novemba 2016
MIKATE YA MAZIWA (MILK BREAD)
MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Unga wa Ngano 550gm
Plain Purpose Flour 550gm
2.Maziwa 300ml
Milk 300ml
3.Sukari Vijiko 4
Sugar 4 Tbsp
4.Hamira Vijiko 2
Yeast 2 Tbsp
5.Chumvi Kijiko Cha Chai 1/2
Salt 1/2 Tea Spoon
6.Mayai 2
Eggs 2
7.Maziwa ya Unga Vijiko 2
Milk Powder 2
8.Ufuta Kijiko 1
Sesame seeds 1 Tbsp
9.Siagi Vijiko 2
Butter 2 Tbsp
10.Unga wa Kusukumia 1/2 Kikombe
Flour for rolling dough 1/2 Cup
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Kwenye bakuli changanya unga,maziwa ya unga,sukari,chumvi na hamira
In a big bowl add flour,milk powder,salt,sugar and yeast
2.Tumia mwiko kuchanganya vizuri
Mix all ingredients in a bowl with spartula
3.Ongeza yai moja,siagi na maziwa ya maji
Add an egg,butter and milk
4.Kanda unga mpaka uwe mlaini na unavutika
Mix all and knead the dough till elastick
6.Ufunike uache uumuke vizuri
Cover the bowl let it rise till double in size
7.Ukisha umuka toa kwenye bakuli ukande kidogo mpaka hewa yote itoke
Fold the dough until all the air is removed
8.Kata kata donge lako kupata vipande vilivyo sawa na yafanye kuwa maduara
Spilt the dough into equal pieces and form into round ball
9.Chukua unga mkavu sukuma madonge kwa urefu kisha yazungushe kuanzia ncha ya kwanza hadi ya mwisho
Use the flour remain and sprinkle to the surface and flatten the balls into long dough then roll it starting from the first end to the last end
10.Rudia kwa madonge yote yalobakia
Repeat till you finish all balls
11.Paka trei yako mafuta au siagi
Grease the tray
12.Panga mikate yako
Keep the bread into the tray
13.Vunja yai lilobakia na pakaa mikate yako
Break the egg remain and brush it on the surface of the bread
14.Nyunyizia ufuta mikate yako acha iumuke kwa dakika 20
Sprinkle the sesame seeds and let them raise for 20 minutes
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Washa Jiko la umeme moto wa juu na chini 180'C
Heat the oven 180'C
2.Oka mikate kwa muda wa dakika 20 mpaka 30
Bake them for 20 to 30 minutes
3.Ikiiva itoe jikoni acha ipoe na itoe kwenye trei yake
When they are ready remove them from the oven let them cool and unmold from the tray
4.Weka kwenye sahani paka siagi tayari kula na kinywaji upendacho
Apply butter after that they are ready to serve with any drinks
Angalizo:Note
1.Hakikisha unakanda unga vizuri hadi uwe mlaini
Make sure you knead the dough till soft
2.Hakikisha mikate inaumuka vizuri kabla kuioka
The breads must be rise well enough before baking
Furahia Mikate Yako
0 comments:
Chapisha Maoni