Jumanne, 22 Desemba 2015

MISHKAKI(BARBEQUE)


MAHITAJI
1.Nyama kilo 1
2.Mafuta kikombe kidogo cha chai 1
3.Tangawizi kubwa 1
4.Kitunguu thomu kikubwa 1
5.Chumvi kiasi
6.Royco pakti 2
7.Binzari nyembamba ya unga(Uzile) vijiko vya chakula 4
8.Ndimu kubwa 2
9.Chumvi kiduchu

MAANDALIZI
1.Kata kata nyama yako vipande ukubwa upendao weka kwenye chombo safi
2.Menya Tangawizi na vitunguu thomu na uvioshe vizuri
3.Saga au twanga Tangawizi na vitunguu thomu
4.Weka mchanganyiko wako kwenye nyama yako ulioikata
5.Weka chumvi pamoja na royco na uchanganye vizuri
6.Ugawe sehemu mbili sawa moja weka cocoa mwengine uache kama ulivyo
7.Kamua ndimu na weka kwenye nyama yako
8.Weka binzari nyembamba changanya vizuri kwa mkono
9.Iweke nyama yako kwenye friji kwa lisaa au zaidi
10.Ukiitoa kwenye friji chukua vijiti safi na chomeka nyama tatu au nne kwenye kijiti kimoja

JINSI YA KUPIKA
1.Chukua jiko la kuchomea nyama
2.Kisha pakaa mafuta kwenye wavu ya kuchomea kwa kutumia brashi
3.Baada ya dakika 1 anza kupanga mishkaki yako kwenye wavu
4.Acha iive kisha igeuze upande wa pili na ipake mafuta tena
5.Acha iive kisha itoe tayari kwa kula
Angalizo:
1.Weka moto mwingi kiasi ili nyama iive vizuri
2.Unapoweka kwenye friji husaidia kulainisha mishkaki
3.Unaweza kuweka karoti kati au viazi mbatata ukipenda
4.Unaweza kuweka masala zaidi za nyama kama unazo pia

Furahia Mishkaki Yako.

0 comments:

Chapisha Maoni