Jumatano, 22 Machi 2017

BANZI LA TUI LA NAZI(COCONUT MILK BREAD ROLLS)


MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Unga wa Ngano Nusu(1/2 Kg)
 1/2Kg All Purpose Flour

2.Tui la Nazi Kikombe Kidogo 1
1 Cup Coconut Oil

2.Samli Vijiko Vikubwa 2
 2 Tbsp Ghee

3.Sukari Vijiko Vikubwa 3
 2 Tbsp Sugar

4.Chumvi Kijiko cha Chai 1
 1 Tea Spoon Salt

5.Hamira Vijiko Vikubwa 2
2 Tbsp Dry Yeast

6.Ufuta Vijiko Vikubwa 2
 2 Tbsp Sesame seeds

7.Mafuta Kijiko Kikubwa 1
 1 Tbsp Cooking Oil

8.Yai Kubwa 1
 1 Large Egg


MAANDALIZI/PREPARATION
1.Weka hamira,unga kijiko 1,sukari kijiko 1,chumvi kiduchu na tui la nazi vijiko 3 kwenye kibakuli au kikombe acha kwa dakika 5 iumuke
 In a small ball/cup add dry yeast,pinch of salt,1 tbsp flour,1 tbsp sugar and 3 tbsp coconut milk mix them and let it rise for 5 minutes

2.Vunja yai kisha litenganishe ute mbali na kiini mbali
 Break an egg and seperate it from egg yolk and egg white

3.Katika bakuli kubwa weka unga,sukari,chumvi na kiini cha yai kisha changanya vizuri sana
 In a large bowl mix the remaining flour,salt,sugar,egg yolk till mixed

4.Changanya hamira ilioumuka pamoja na unga
 Pour the risen yeast in the flour mixture

5.Weka tui kidogo kidogo mpaka unga ushikane uwe donge moja 
  Pour the coconut milk slowly until you get a fine dough

6.Kanda unga kiasi cha dakika 10 kisha weka samli kijiko 1 endelea kukanda hadi uwe mlaini
 Knead the dough for at least 10 minutes then add a tbsp of ghee and keep kneading till soft

7.Ukusanye uwe donge moja la duara na pakaa samli donge lote hadi lienee
 Keep the dough into circle and apply the remaining ghee on top of it

8.Funika unga kwa kitambaa kisafi kisha uache uumuke kwa dakika zisizo pungua 20.
 Cover the dough and let it rise for 20 minutes

9.Ukande tena kidogo kisha kata madonge nane yafanye yawe duara
 Slightly knead the dough and then cut it into 8 pieces and roll them into ball shape

10.Chukua chombo cha kuokea kipake mafuta
 Grease the baking tray with some oil

11.Panga madonge na hakikisha unaacha nafasi baina yao aacha yaumuke kwa muda wa dakika 30 
 Place the dough in the baking tray make sure you leave a space between them and let the balls rise for 30 minutes

12.Baada ya kuumuka pakaa kiini cha yai juu ya madonge yako na nyunyizia ufuta
  Apply egg white on top of the balls and sprinkle the sesame seeds

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Washa jiko la umeme moto wa 180
 Heat the oven 180'C

2.Oka banzi zako kwa muda wa dakika 20
 Bake them for 20 minutes

3.Zikiiva toa kwenye jiko na uzipake mafuta
 Remove them from the oven and apply some oil on top of the balls

4.Acha zipoe tayari kwa kuliwa na kinywaji upendacho
 Let them cool you can serve with any drinkyou prefer

Angalizo:Note;
1.Ili banzi ziwe lainii hakikisha unakanda unga hadi unakuwa mlainii kabisa
 Make sure you knead the dough till soft so as to get very soft bread

2.Banzi nzuri lazima ziachwe ziumuke zaidi ya nusu saa
 Make sure you give them enough time to rise before bake them

3.Kama jiko lako linaunguza hakikisha unaweka moto wa wastani kulingana na jiko lako
 Set the oven heat according to your oven to avoid the bread to get burnt

4.Unaweza kupika za chumvi tu, unaweka chumvi kijiko cha chakula kimoja bila kuweka sukari na kiini chai,mahitaji yalobakia unaweka kama hapo juu yalivyo orodheshwa
 You can make them by using salt only,by adding one table spoon of salt and all ingredients mentioned above except sugar and egg yolk.

5.Kwa wanaotumia mkaa unaweza kuoka kwa mkaa pia
  You can bake them by using Charcoal stove

6.Mafuta yanayopakwa baada ya banzi kuiva lazima yasiwe na harufu yoyote
  Oil applied on top of buns must be free from bad smell 

7.Unaweza kupaka siagi kama mbadala wa mafuta baada ya kuzitoa jikoni
   You can apply butter instead of cooking oil once it is taken from the oven


Furahia Banzi Zako.Enjoy your Buns

2 comments:

Aroma of Zanzibar alisema ...

Mashallah banzi nzuri sana

Unknown alisema ...

Shukran Sis Aroma Of Zanzibar Tunafata nyayo zako

Chapisha Maoni