Jumatano, 10 Februari 2016

CHIPSI ZA MUHOGO(FRIED CASSAVA CHIPS)


MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Mihogo 5
  5 Fresh Cassava

2.Mafuta lita 1
  1 Litre Cooking Oil

3.Chumvi kijiko 1
  1 Tbsp Salt

MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Menya mihogo yako na ikoshe
Peel the cassava and wash them 

2.Chukua kipario cha karoti para mihogo kisha itandaze kwenye sinia acha zikauke kwa lisaa1
   Grate them by using grater once you finish put the chips into the big plate and let them dry for at least an hour 

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka mafuta kwenye karai acha yapate moto
  Heat the oil to the maximum into the big frying pan

2.Zigawe mafungu matatu chipsi zako mbichi
  Group the dried chips into three groups

3.Kisha weka fungu la kwanza kuwa makini mafuta huwa yanakuja juu
  Add the first group into the pan becareful with heated oil since it rise when you insert the chips

4.Acha zishikane mpaka chini zipige rangi ya dhahabu
  Let them fry until combine and started changing to golden colour at the bottom part

5.Geuza chipsi zako upande wa pili acha nao uive
  Flip to the other side until cooked

6.Zikiwa tayari zitoe weka kwenye chujio zichuje mafuta
 When they are done in both sides remove them and keep them into the sieve

7.Acha zipoe kisha zivunje vunje taratibu weka chumvi 
  When they are completely cool break them slowly and add salt then mix them well

8. Unaweza kula na pilipili ya unga au chatne,karanga za kukaanga(njugu za kukaanga) au weka kwenye urojo
Ready to serve with chili powder or fried peanut or urojo (recipe available in my blog) or chatne(recipe available in BADIA'S POST)

Angalizo:Note;
1.Acha chipsi zikauke kabla ya kuzipika ukiweka mbichi zina nyonya mafuta
  Make sure the grated chips are dried enough before you fried them other wise they will absorb a lot of oil during frying

2.Kuwa makini zisiungue kwani zikiungua zinakua chungu
 Make sure they are not get burnt otherwise the taste will turn into sour


Furahia Chipsi Zako

1 comments:

Unknown alisema ...

Mihogo inatakiwa ikauke kwa kiwango gani?

Chapisha Maoni