MAHITAJI
1.Mchele robo kilo
2.Nazi 1
3.Samaki kibua wa kukaanga 2
4.Nyanya(Tungule) kubwa 3
5.Karoti kubwa 1
6.Pilipili hoho(Pilipili boga) 1
7.Kitunguu maji kikubwa 1
8.Kitunguu thomu
9.Maji kiasi
10.Chumvi
11.Ndimu
12.Bamia
13.Nyanya chungu
14.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Chagua mchele vizuri kisha ukoshe na weka pembeni
2.Para au saga nyanya weka pembeni
3.Kata kata kitunguu maji weka pembeni
4.Twanga kitunguu thomu weka pembeni
5.Kata karoti na pilipili boga ndefu ndefu
6.Kuna nazi na weka tui jepesi na zito kwa ajili ya mchuzi
JINSI YA KUPIKA
WALI
1.Weka maji na chumvi jikoni yakichemka weka mchele
2.Subiri maji yakauke geuza na pambia wali wako(Nishaelekeza jinsi ya kupika wali kwenye post zanyuma)
3.Ukiiva acha upoe ili uje kuupakua vizuri
MCHUZI
4.Weka samaki ulowakaanga kwenye chombo cha kupikia mchuzi wako
5.Weka bamia,nyanya chungu,kitunguu maji,kitunguu thomu,chumvi,karoti,pilipili boga na nyanya pamoja na maji kidogo kwenye samaki wako
6.Wacha vichemke kisha weka ndimu ulio ikamua acha kwa dakika 1
7.Anza kuweka tui jepesi acha lichemke mpaka lipungue
8.Malizia kuweka tui zito acha uchemke mpaka uwe mzito mzito kwa dakika 4 kisha uepue
9.Unaweza kula na wali,ugali,mkate n.k
JINSI YA KUANDAA
1.Chukua kibakuli kidogo
2.Weka wali wako kiasi
3.Weka kwenye sahani upendayo
4.Pakua mchuzi na umimine kwa juu
5.Weka samaki wako pembeni tayari kwa kula
Angalizo:
1.Epuka kuweka maji mengi kwenye mchuzi wako
2.Epuka kukoroga mara kwa mara
Furahia Mchuzi na Wali Wako.
0 comments:
Chapisha Maoni