Jumatano, 2 Desemba 2015
MIHOGO YA KUCHEMSHA NA SAMAKI WA KUKAANGA(BOILED CASSAVA WITH FRIED FISH)
MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Mihogo Vipande 12
Fresh Cassava 12 pieces
2.Samaki(Changu wadogo) 4
4 Fresh Changu fish
3.Maji Nusu Lita
Water 500ml
4.Chumvi Vijiko Vya Chakula 2
Salt 2 tbl spoon
5.Mafuta ya kupikia Kikombe 1
Cooking Oil 1 cup
7.Pilipili Vijiko 4 Ukipenda
Chilli sauce(Option) 4 tbl spoon
8.Kachumbari Bakuli 1
Salad 1 bowl
9.Pilipili Ya kuwasha 2
Red Pepper 2
10.Ndimu Vijiko Vya Chakula 4
Lemon juice 4 tbl spoon
11.Vitunguu thomu Punje 3
Garlic 3 pieces
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Osha samaki vizuri baada ya kuwasafisha kisha waweke kwenye bakuli
Wash the fishes and kept them in a big bowl
2.Twanga kitunguu thomu na pilipili na chumvi
Mash the garlic with pepper and salt
3.Weka viungo ulivyotwangwa kwenye samaki
Marinate your fishes with pepper mixture
4.Ongeza ndimu kisha wachanganye vizuri
Add lemon juice and mix them well
5.Menya mihogo na ikoshe vizuri
Peel the cassava and wash them
7.Kata mihogo kupata vipande 12
Cut the cassava in 12 pieces
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
MUHOGO/CASSAVA
1.Weka mihogo kwenye sufuria pamoja na maji na chumvi
Keep the cassava in a pot(cooking dish) with salt and water
2.Chemsha hadi mihogo iwive na kuwa laini
Boil them until cooked and smooth
3.Mwaga maji yaliobakia kwenye mihogo na iwe mikavu
Pour or remove excess water remained in a pot
4.Weka mihogo kwenye sahani
Keep them in a plate
SAMAKI WA KUKAANGA/FRYING FISH
1.Weka mafuta kwenye kikaangio
Take a frying pan and put some oil
2.Weka kikaangio jikoni weka moto mkali
Keep the pan on stove on high heat
3.Baada ya dakika 3 weka samaki
Leave it for 3 minutes and put your fishes
4.Baada ya dakika 5 wageuze samaki upande wa pili
After 5 minutes flip the fishes in another side and let it cooked
5.Waache kwa dakika 5 nyengine
Leave it for another 5 minutes
6.Toa samaki wako waweke kwenye tissue au chujio wachuje mafuta
Remove your fishes and keep them on the tissue
7.Baada ya dakika 3 wako tayari kuliwa
After 3 minutes they can be served
8.Kula samaki na mihogo pamoja na kachumbari na pilipili
Serve them with your boiled cassava and chilli sauce and salad
9.Unaweza kula na chai au uji ukipenda
You can use tea or porridge too if you wish
Furahia Muhogo na Samaki wako.
2 comments:
wooow delicious
Ahsante Flora Msofe
Chapisha Maoni