MAHITAJI
1.Ndizi Malindi 6
2.Viazi Mbatata 2
3.Nyanya(Tungule) 3
4.Karoti 1
5.Pilipili Boga(Pilipili hoho) 1
6.Kuku robo
7.Tangawizi ilosagwa kijiko kidogo cha chai 1
8.Kitunguu maji 1
9.Kitunguu thomu punje 4
10.Chumvi kijiko 1
11.Maji nusu lita 2
13.Pilipili ya unga au pilipili yoyote
MAANDALIZI
1.Weka Maji lita 1 kwenye beseni tumbukiza ndizi zako hii husaidia kuondosha utomvu na kumenya kiurahisi
2.Weka nusu lita kwenye bakuli
3.Menya ndizi weka zipare kidogo weka kwenye lile bakuli
4.Kata ndizi sehemu tatu sawa
5.Menya viazi na vioshe
6.Vikate kwa urefu sehemu mbili sawa
7.Kisha vichanganye na ndizi
8.Menya na kuviosha Nyanya,Kitunguu maji,kitunguu thomu,pilipiliboga na karoti
9.Kata kata Kitunguu maji,pilipili boga,karoti kwa umbo upendalo
10.Para au saga nyanya weka pembeni
12.Twanga kitunguu thomu na chumvi kiduchu weka pembeni
13.Osha kuku wako vizuri kisha muweke pembeni kwenye chombo safi
JINSI YA KUPIKA
1.Teleka sufuria ya ndizi jikoni weka maji yaliobaki na chumvi kiasi
2.Mimina viungo ulivyo vikatakata kwenye ndizi
3.Weka kuku,tangawizi na kitunguu thomu kwenye ndizi
4.Acha vichemke kwa dakika 5 huku ukiwa umezifunika
5.Malizia kuweka nyanya ulizo zisaga acha kwa dakika 5 nyengine
6.Toa ndizi angalia kama imeiva epua weka kwenye sahani
7.Subiri kipoe tayari kwa kula
Angalizo:
1.Usikoroge upishi tumia banio la ugali kutikisa au kitambaa kisafi cha jikoni
2.Tumia moto wa kati na kati usipikie moto mwingi zitaganda kwenye sufuria
3.Hakikisha kuku hakai chini ili asivurugike labda awe wa kienyeji
Furahia Mchemsho Wako
1 comments:
Maa Shaa Allah nimeipenda hii
Chapisha Maoni