Jumatatu, 7 Desemba 2015
NJUGU MAWE ZA SUKARI
MAHITAJI
1.Njugu mawe robo kilo
2.Nazi 1
3.Hiliki punje 10
4.Sukari vijiko vya chakula 5
5.Custard kijiko cha chai kimoja
6.Arki (Vanilla)kijiko cha chai 1
7.Chumvi kiduchu
MAANDALIZI
1.Chagua njugu mawe zako toa mawe yote
2.Weka kwenye chombo na uzikoshe vizuri
3.Kuna nazi na chuja nazi tui zito kikombe kikombe kidogo cha chai na kisha lilobakia chuja kibakuli
kimoja tui jepesi
4.Menya na kutwanga na sukari kiduchu hiliki yako
5.Weka custard kwenye tui lako zito kisha weka pembeni
JINSI YA KUPIKA
1.Weka njugu zako kwenye sufuria na maji kiasi
2.Chemsha njugu zako maji yakikauka weka maji kidogo kidogo ili njugu zako ziwive vizuri
3.Njugu zikiwiva mimina tui jepesi,hiliki,sukari na chumvi
4.Acha tui lipungue kisha mimina lile tui zito na arki
5.Acha lichemke kidogo na ikiwa nzito nzito epua
6.Unaweza kula na Chapati,Mkate wa ufuta,Boflo au mkate wowote
Angalizo:
1.Wakati wa kuchemsha njugu usiweke maji mengi ili zisivurugike na kubanduka maganda na kupelekea kuto kuiva
2.Usiweke custard nyingi inasababisha kuwa nzito zaidi na kupoteza ladha yake
3.Hakikisha hauweki tui jingi jepesi ili ziwe nzito na tamu
4.Usikoroge upishi wako mpaka una maliza kama ukitaka kuchanganya chukua banio la ugali ushikie sufuria yako kisha itikise au tumia kitambaa kisafi cha jikoni ushikie sufuria yako kisha itikise
Furahia Njugu Mawe Zako.
0 comments:
Chapisha Maoni