MAHITAJI:
1.Mchele wa basmat nusu
2.Kuku nusu
3.Vitunguu Maji 3(vikubwa)
4.Vitunguu thomu punje 7(Kubwa)
5.Nyanya(Tungule) 1 Kubwa
6.Viungo vya pilau vizima(Mdalasini,Pilipili-Manga,Binzari nyembamba(Uzile),Hiliki)Kiasi Upendacho.
7.Karoti Kubwa moja
8.Pilipili Hoho(Pilipili Boga) moja
9.Viungo vya Pilau vya Unga Mchanganyiko(Mdalasini,Pilipili-Manga,Binzari nyembamba(Uzile),Hiliki) Vijiko Vitatu vya cha Chakula.
10.Mafuta ya kula Kiasi
11.Chumvi Kiasi
12.Tangawizi KIasi
13.Maji Kiasi
14.Viazi Mbatata 8
15.Zabibu Kavu Kiasi Upendacho.
16.Njegere Nusu Glasi.
MAANDALIZI:
1.Katakata Kuku Jinsi Upendavyo Kisha muoshe.
2.Menya Kitungu thomu punje 2 na Tangawizi kiasi Kisha vitwange kwa pamoja na chumvi(kwa Matumizi ya Kuweka Kwenye Kuku).
3.Menya Viazi na vioshe kisha viweke Pembeni.
4.Osha Mchele wako vizuri na uweke Pembeni.
5.Twanga Kitungu Maji Kimoja,Vitungu thomu Vilivyobaki Pamoja na Chumvi.
6.Katakata vitunguu maji vilivyobakia,Pilipili hoho na Uipare Karoti yako.
7.Para nyanya yako na uiweke Tayari kwa Kupika.
8.Loweka Viungo vya pilau vizima kwenye maji Kiasi.
9.Osha njegere zako ziwe tayari.
JINSI YA KUPIKA:
1.Weka Kuku wako pamoja na viungo ulivyovitwanga(thomu na Tangawizi) kwenye Sufuria Kisha acha dakika 1 halafu chemsha na maji kiasi.
NB:
-Kwa kuku wa Kisasa Chemsha kwa Dakika Tano kisha Muache na Supu Yake.
-Kwa Kuku wa Kienyeji Chemsha Mpaka atakapo Iva Kisha Muache na supu yake.
2.Chukua Sufuria weka mafuta ya kupikia na uyaache ya Pate Moto Kiasi.
3.Kaanga Vitungu maji Mpaka viwe na rangi ya brown.
4.Weka Pilipili Hoho na umalizie Na Karoti,acha kidogo.
5.Weka Nyanya yako uliyoipara kwenye Mchanganyiko wako na koroga Kidogo.
6.Weka Viazi Kwenye Mchanganyiko wako na Ukaange Kidogo.
7.Weka mchanganyiko wa vitunguu thomu na vitunguu Maji ulivyovitwanga kwenye Mchanganyiko wako.
8.Weka Viungo vya pilau vya unga kwenye Mchanganyiko wako.
9.Weka viungo vya Pilau Vizima ulivyoloweka kwenye Mchanganyiko wako.
10.Weka Njegere Kwenye Mchanganyiko wako.
11.Weka Kuku pamoja na supu yake.
12.Ongeza Maji Kiasi kwenye mchanganyiko wako ili uendane na Kiasi cha Mchele wako,Kisha Ongeza Zabibu Kavu.
13.Angalia Kiasi cha Chumvi kwenye Mchanganyiko wako.Kama Kidogo ongeza Kiasi Upendavyo.
14.Acha kidogo Vichemke.
15.Weka Mchele kwenye Mchanganyiko wako Koroga Kidogo Kisha Funikia.Tumia Moto mdogo kiasi ili pilau lako lisije Kuungua kwa mnao tumia gesi.
16.Maji yakisha Kaukia Funua na changanya pilau lako vizuri kisha funika tena.
17.Subiri kama dakika tano na funua kuangalia kama mchele wako umeshaiva.
18.Kama wali wako Umeiva,Pishi lako la pilau litakuwa tayari kwa kuliwa na kachumbari(salad).
NB:
-Ili Pilau liwe zuri na linukie hakikisha viungo vya pilau vya unga Umetengeneza mwenyewe.
-Pia unaweza Kutumia Pilau Masala kama hauna Mchanganyiko wa viungo vya Unga.
-Pia unaweza kuweka viungo zaidi kwenye kumuunga kuku upendavyo.
0 comments:
Chapisha Maoni