MAHITAJI
1. Blue band robo
2.Sukari robo(kama sio mpenzi wa sukari usiweke yote)
3.Unga nusu
4.Cocoa kikombe kimoja
5.Zabibu kavu kiasi
6.Maziwa kikombe kimoja
7.Baking powder kijiko kimoja
8.Mayai 5
9.Arki vanilla kijiko kikubwa kimoja
10.Chumvi kiduchu
MAANDALIZI
1.Chunga unga na uweke chumvi na baking powder
2.Chukua chombo weka Blue band na sukari
3.Saga mchanganyiko wako kama una mashine ya kusagia keki(hand mixer au stand mixer)kwa dakika 5 au dakika kumi kwa kutumia mwiko
4.Chukua bakuli vunja mayai na uyaweke kwenye mchanganyiko wako
5.Endelea kusaga mpaka kwa dakika 5 kisha weka arki yako.
6.Weka maziwa na usage tena kwa dakika 5
7.Chukua unga anza kuweka kidogo kidogo mpaka upate uji uji mzito kiasi
8.Weka zabibu kisha ugawe mchanganyiko wako sehemu mbili sawa sawa
9.Sehemu moja weka cocoa nyengine iache vile vile
10.Changanya vizuri ule mchanganyiko uliouweka cocoa.
11.Chukua tray au chombo cha kupikia weka Blue band au karatasi ya kupikia ndani
12.Kisha chota mchanganyiko wa cocoa kijiko kimoja weka kati kati ndani ya chombo cha kupikia ikifuatiwa na mchanganyiko mweupe.Au unaweza kuanza mweupe ukafatiwa na wa cocoa.
13.Rudia njia hio mpaka umalize mchanganyiko wako.
JINSI YA KUPIKA
1.Washa oven yako moto wa wastani kati ya 120' au 150'(inategemea na jiko lako)
2.Weka keki yako na iache kwa dakika 10
3.Endelea kuiangalia mpaka itakapo iva
4.Kuangalia kama imeiva ndani chukua kijiti kisafi chomeka sehemu tofauti kwenye keki yako kikitoka kikavu basi imeiva ndani na kikiwa kibichi keki haijaiva endelea kuipika.
5.Ikiiva kata kata keki yako tayari kula kwa Juice,Chai,Maziwa,Maji.
NB: Keki ni upishi unaotakiwa kuangaliwa mara kwa mara ili isije kuungua kwa hio kua makini wakati wa kuipika.
Furahia Keki Yako.
0 comments:
Chapisha Maoni