MAHITAJI
1.Mchele wa Basmat
Robo(1/4 kg)
2.Mafuta ya kula robo
lita
3.Kitunguu maji kikubwa
1
4.Karoti kubwa 1
5.Pilipili
Hoho(Pilipili boga) kubwa 1
6.Chumvi vijiko vikubwa
2
7.Uzile mzima(Binzari
Nyembamba) kijiko kidogo 1
8.Mdalasini mzimakijiko
kidogo 1
9.Hiliki punje 10
10.Giligilani nzima
punje 15
11.Viazi Mbatata vidogo
8
MAANDALIZI
1.Osha mchele wako
vizuri uweke pembeni
2.Katakata kitunguu
maji,karoti na pilipili kila kimoja kata kwenye sehemu yake
usivichanganye
3.Menya viazi mbatata
kisha kata kata kwa umbola chipsi.
JINSI YA KUPIKA
1.Chukua sufuria weka
maji na chumvi kijiko 1 yakichemka weka mchele wako acha uchemke na
uive kidogo kisha umwage maji uache bila maji.
2.Chukua sufuria weka
viungo vya pilau(Mdalasini,hiliki,giligilani na uzile) vikaange bila
mafuta mpaka vitoe harufu epua viweke pembeni
3.Chukua sufuria
nyengine uweke mafuta na kaanga chipsi mpaka ziive kisha zitoe
4.Ukitoa chipsi anza
kukaanga vitunguu maji mpaka viwe brown kiasi kisha vitoe,halafu
kaanga keroti na uzitoe na malizia kukaanga pilipili boga na kisha
zitoe
5.Chukua chombo yatoe
yale mafuta yote uliokaangia na bakisha sufuria tupu
6.Mimina wali uliopika
kwenye ile sufuria kidogo kisha juu weka viazi mbatata,kisha ongeza
wali kidogo juu ya viazi mbatata kisha weka pilipili boga
ulilolikaanga kisha mimina wali juu weka vitunguu maji na rudia hivyo
hivyo mpaka mwisho juu kabisa weka vile viungo vya pilau.
5.Nyunyizia chumvi
kijiko kimoja juu ya wali wako
6.Mimina yale mafuta
kidogo uliyo tumia kukaangia viungo vyako kisha ufunike wali wako
upate kukauka
7.Acha wali ukauke kwa
moto mdogo kwa dakika 5 usiukoroge.
8.Baada ya huo muda
kupita uepue kisha uchanganye na upakue
9.Unaweza kula kwa
rosti zito zito kama la maini,nyama au kuku
Angalizo:
1.Pangilia vizuri wali
kwa kutenganisha na viungo vyako
2.Sio lazima upange
kama nilivyo orodhesha hapo juu ila ni muhimu kutenganisha viungo na
wali wako
3.Usiukoroge mpaka
wakati wa kuupakua
Furahia Wali Wako.
0 comments:
Chapisha Maoni