MAHITAJI
1.Mchele wa Basmat nusu kilo(1/2 kg)
2.Mafuta kiasi
3.Viazi mbata vidogo 10
4.Mayai 3
5.Sosej 3
6.Vitunguu maji vikubwa 2
7.Karoti kubwa 1
8.Njegere kikombe 1
9.Green Beans 4
10.Pilipili Boga
11.Maji kiasi
12.Chipsi
MAANDALIZI
1.Menya viazi vioshe na vikate kwa umbo la chipsi
2.Katakata keroti mbali,pilipili boga mbali,vitunguu maji mbali
3.Osha njegere weka pembeni
4.Osha mchele weka mbali
5.Kata sosej vipande vidogo vidogo weka pembeni
JINSI YA KUPIKA
1.Weka maji,njegere na chumvi weka jikoni acha yachemke kisha weka mchele acha uive kidogo sana
2.Ukiiva kidogo epua na umwage maji yote uwe mkavu
3.Weka karai mafuta yakipata mafuta kaanga chipsi zikiiva epua weka pembeni
4.Vunja mayai weka chumvi kidogo kisha yakaange likiiva weka kwenye saghani acha lipoe kisha likate vipande vidogo vidogo vya pembe nne
5.Teleka sufuria na weka mafuta yakipata moto kaanga vitunguu maji vikiwa brown weka keroti kisha pilipili boga halafu sosej kisha mayai,green beans na malizia na chipsi
6.Weka chumvi koroga mchanganyiko wako vizuri
7.Chukua wali uliopika ugawe sehemu 2 sawa kisha nusu weka kwenye mchanganyiko wako na ukoroge vizuri sana.
8.Kisha malizia kumimina wali uliobaki juu ila usikoroge funika wali wako na uache ukauke
9.Wali ukikauka epua uchanganye vizuri kisha pakua
10.Unaweza kula na nyama ya kuku wa kukaanga
11.Pia unaweza kupamba na kula na mayai ya kuchemsha kama hapo kwenye picha yangu
Angalizo;
1.Hauwekwi kitunguu thomu
2.Unakorogwa mara moja tu baada ya kuweka nusu ya wali
3.Usiweke mafuta mengi sana wakati wa kukaanga utaubadilisha ladha na rangi
4.Hauliwi na mchuzi ila kama una watoto nyumbani unaweza kuwafanyia mchuzi mzito mzito
Furahia Wali Wako.
0 comments:
Chapisha Maoni