Jumanne, 26 Januari 2016

MIKATE YA UFUTA


MAHITAJI
1.Unga wa ngano nusu
2.Nazi kubwa 1
3.Hamira vijiko vya chakula 2
4.Chumvi kijiko cha chakula 1
5.Mafuta nusu kikombe cha chai
6.Ufuta nusu kikombe cha chai
7.Maji kiasi

MAANDALIZI
1.Kuna nazi na chuja kwenye chombo ujazo wa jagi dogo la maji
2.Chekecha unga wako vizuri kwenye bakuli safi
3.Weka chumvi na uchanganye unga vizuri kisha weka tui kidogo kidogo huku ukichanganya kwa mkono
4.Endelea kuweka tui mpaka unga uwe kama uji uji sio mzito sana wala mwepesi sana
5.Acha kuweka tui fanya kama unaupiga piga makofi kutoa mabuje na mabonge kwa muda wa dakika 10
6.Uache unga wako ufure na uumuke vizuri

JINSI YA KUPIKA
1.Andaa jiko la mkaa lenye moto wa wastani
2.Weka maji na chumvi kidogo kwenye kibakuli kinachoweza kuingia mkono
3.Chukua chuma(Frying pan) cha kupikia ufuta weka mkono kwenye maji ya chumvi kisha fanya kama unakungutia maji yaloganda kwenye mkono katika chuma chako
4.Chota kwa mkono uji wako weka kama mikono miwili ya uji kwenye chuyma cha mkate
5.Kiweke jikoni kisha chukua ufuta kiasi nyunyizia juu ya ule uji kwenye chuma chako
6.Acha kwa dakika 3 ukiona unaanza kubadilika kuwa na weupe wa kuiva kwa chini geuza chuma cha mkate juu chini kama unataka kuumwaga mkate
7.Weka chuma hivyo hivyo huku ukiuangalia mkate wako usiungue
8.Ukiwa wa brown geuza chuma kisha tumia kisu kutoa mkate wako
9.Weka kwenye sahani chukua brush chovya kwenye mafuta kisha upake mkate wako kwa kupakaa mafuta kidogo tu
10.Rudia njia hizo hapo juu mpaka umalize uji wako wote.
Angalizo:
1.Hakikisha unatumia vyuma vya bati(Frying pan za Bati) vinavyotengenezwa Tanzania ndio vya kupikia mikate ya ufuta ukitumia chuma kingine mkate utaanguka kwenye moto
2.Pia mkate huu unapikwa kwa kutumia jiko la mkaa au wengine wanatumia grill
3.Tumia moto wa wastani kupata rangi ya kuvutia mkate ukiungua hup[oteza rangi ya mvuto na ladha hubadilika

4.Halkikisha huzidishi chumvi wakati wa kupika hufanya mikate kuwa mibaya
5.Ili mikate iwe milaini hakikisha tui linakua zito na  la kutosha

Furahia Mikate Ya Ufuta.

0 comments:

Chapisha Maoni