Jumanne, 26 Januari 2016

KISAMVU


MAHITAJI
1.Mboga ya Kisamvu kiasi
2.Nazi ndogo moja
3.Karoti ndogo 1
4.Kitunguu maji 1
5.Kitunguu thomu punje 5
6.Pilipili boga(Pilipili hoho) ndogo 1
7.Nyanya kubwa(Tungule) 1
8.Sukari kijiko kidogo 1
9.Chumvi vijiko kikubwa 2
10.Maji kiasi

MAANDALIZI
1.Osha mboga yako vizuri kisha iweke kwenye kinu
2.Twanga mboga yako na chumvi kijiko kimoja na kitunguu thomu
3.Twanga mpaka itwangike vizuri kisha weka kwenye sufuria
4.Kuna nazi kisha chuja tui la kwanza na la pili
5.Osha viungo vyako kisha katakata vitunguu maji,nyanya,pilipili hoho na karoti ipare

JINSI YA KUPIKA
1.Weka mboga jikoni na maji kiasi acha ichemke
2.Maji yakikauka weka mengine chemsha mboga yako kwa muda wa dakika 20
3.Ikiiva weka viungo ulivyo vikata kata na tui la kwanza acha vichemke
4.Baada ya tui kupungua onja mboga yako kama chumvi hakuna au imepungua ongeza
5.Kisha weka sukari na tui la kwanza acha likaukie ila libaki kiduchu sana
6.Likikauka epua ichanganye vizuri
7.Weka kwenye kibakuli unaweza kula na wali,ugali,chapati n.k
Angalizo:
1.Ni vizuri mboga kuichemsha sana kabla ya kuweka nazi
2.Hakikisha unaweka nazi ya kukuna mwenyewe ili mboga iwe tamu
3.Usikaushe mboga kabisa kabisa na wala usiiwache na maji mengi
4.Ukipenda chemsha mboga yako na kunde au mbaazi mbichi

Furahia Kisamvu Chako

0 comments:

Chapisha Maoni