MAHITAJI
1.Blue band robo
2.Sukari robo
3.Mayai 6
4.Baking powder
kijiko cha chakula 1
5.Unga wa ngano nusu
9.Arki Vanilla
kijiko 1
10.Arki ya Ice cream
kijiko 1
11.Fruit za keki
robo kikombe cha chai
12.Chumvi kiduchu
13.Sukari ya Dandii
robo kikombe kidogo cha chai
MAANDALIZI
1.Chunga unga wa
ngano weka baking powder na chumvi uchanganye weka pembeni
2.Saga sukari na
siagi(Blue band) kwa mkono au hand mixer mpaka ilainike
3.Koroga vizuri
kisha weka arki na uchanganye vizuri
4.Vunja mayai weka kwenye mchaganyiko wako wa siagi
4.Vunja mayai weka kwenye mchaganyiko wako wa siagi
5.Weka unga taratibu
mpaka mchanganyiko wako uwe uji mzito
6.Weka dandii yako
na changanya vizuri mchanganyiko wako
7.Malizia kwa kuweka
fruit kisha koroga vizuri
8.Weka kwenye tray
au chombo chochote cha kupikia keki
JINSI YAKUPIKA
1.Washa oven kwa
moto wa wastani
2.Weka keki yako
acha iive mpaka ipige rangi ya brown
3.Chukua kijiti
kisafi au tooth pick
4.Chomeka sehemu
tofauti kuangalia kama keki imeiva
5.Kijiti kikitoka
kikavu keki imeshaiva
6.Kikitika kimaji
iache keki ikauke
7.Toa keki ikiiva
kata kata tayari kula na Kinywaji upendacho
Angalizo:
1.Hakikisha unaweka
moto ambao hauunguzi keki yako
2.Usiweke dandii
nyingi keki itakua chungu
3.Usiweke maji
4.Kama unatumia
mwiko ni vizuri kutumia mwiko wa ugali kusagia keki yako
5.Hakikisha unaisaga
siagi hadi inalainika kama unatumia mkono
6.Unaweza kupika
hata kwa mkaa ukikosa oven
Furahia Fruit
Cake Yako Zako.
0 comments:
Chapisha Maoni