Jumatano, 10 Agosti 2016
MCHUZI WA NAZI WA PWEZA(OCTOPUS COCONUT MILK SAUCE)
MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Pweza nusu kilo
1/2 Kg Octopus
2.Tui Jepesi Kikombe Kikubwa 1
1 Mug Light Coconut Milk
3.Tui Zito Kikombe Cha Chai 1
1 Cup Heavy Coconut Milk
4.Nyanya za Mchuzi(Tungule) kubwa 3
3 Medium Size Tomato
5.Kitunguu maji Kikubwa kiasi 1
1 Medium Size Onion
6.Kitunguu thomu Punje 2 Kubwa
2 Garlic Cloves
7.Tangawizi Kipande Kidogo 1
1 Small Piece Ginger
8.Keroti Kubwa Kiasi 1
1 Medium Size Carrot
9.Pilipili Boga Kubwa Kiasi 1
1 Medium Size Green Pepper
10.Pilipili Ya Kuwasha 1
1 Chilli
11.Chumvi Kiasi
Salt to taste
12.Royco Kijiko Cha Chakula 1(Sio Lazima)
1 Tbsp Royco(Optional)
13.Bamia 5
5 Ladies Finger
14.Nyanya ya Paketi(Tomato Paste) Kijiko Cha chakula 1
1 Tbsp Tomato Paste
15.Ndimu ilokamuliwa 1
1 Squeezed Lemon
16.Maji Kiasi
Some Water
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Osha Viungo vyote vizuri
Rinse well all ingredients with clean water
2.Kwenye jagi la blenda weka Nyanya ulizozikata,Pilipili boga,tangawizi,kitunguu thomu,kitunguu maji
Chop the tomato,onion,green pepper,garlic cloves,ginger then add into the jug of blender
3.Saga mchanganyiko mpaka uwe usagike
Blend the mixture untill mixed
4.Kata keroti katika umbo la duara weka pembeni
Chop the carrot into the circular shape
5.Osha na msafishe pweza vizuri
Rinse and clean the octopus well
6.Mkate kate weka kwenye sufuria
Cut the octopus into the pieces you prefer
7.Kata ncha za bamia kisha likate bamia katikati upate vipande viwili utapata vipande kumi kwa mabamia 5
Cut the ends of ladies finger and then cut it into halves so as finally you get 10 pieces from 5 ladies finger
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka sufuria ya pweza jikoni usiweke maji wala chumvi acha achemke kwanza
In a pot add the octopus pieces let it boil without salt or water for some seconds
2.Utaona anakuwa mwekundu ongeza maji aive mpaka awe mlaini
When it turns to red add some water keep boiling till tender
3.Akiiva mimina mchanganyiko wa nyanya kwenye pweza
When it done add the tomato mixture
4.Acha ichemke kisha ongeza chumvi na ndimu
Let it boil and add salt into the mixture
5.Koroga na weka keroti,bamia na nyanya ya paketi na ukoroge
Add carrots pieces,ladies finger and tomato paste then stir the mixture
6.Mimina royco na ukoroge acha uchemke kidogo
Add royco and stir the mixture
7.Weka tui jepesi na pilipili ikiwa nzima acha lichemke mpaka lipungue usikoroge
Add chilli then pour light coconut milk let it boil till the level of the sauce is little reduce but don't stir it any more
8.Kisha mimina tui zito acha lichemke mpaka lipungue na kuwa zito zito
Pour the heavy coconut milk until the sauce becomes heavy
9.Epua acha upoe kidogo
Let it slightly cool
10.Unaweza kula na wali,ugali au mkate upendao.
You can serve with rice,ugali or breads
Angalizo:
1.Usiweke maji mengi wakati wa kusaga mchanganyiko wa Nyanya na viungo vyengine
Do not add too much water when you blend the tomato with other ingredients
2.Ukisha kuweka Tui usikoroge mpaka mchuzi uwive
Do not stir the mixture once you add coconut milk
3.Usimuweke Chumvi wakati wa kuchemsha huwenda akawa na chumvi nyingi kwasababu pweza ana chumvi yake mwenyewe
Do not add salt when you boil the octopus it may result the sauce to be too salty since the octopus has salt in it
Furahia Mchuzi Wa Pweza.
0 comments:
Chapisha Maoni