MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Siagi 250gm
Margarine 250gm
2.Sukari Vikombe 2 vya Rice Cooker
Sugar 2 Cups(Rice Cooker Cup)
3.Unga wa Ngano vikombe 5 vya Rice Cooker
Plain Flour 5 Cups(Rice Cooker Cup)
4.Jam Robo Kikombe Cha Chai
Jam 1/4 Small Cup
5.Karanga(Njugu) Zilopikwa Kikombe kidogo Cha Chai 1
Baked Groundnuts 1 Small Cup
6.Baking Powder kijiko cha Chakula 1
Baking Powder 1 Tbsp
7.Arki Pine Apple Nusu Kifuniko
Pine Apple Essence 1/2 Cap(Caps of Pine Apple Essence Bottle)
8.Mayai 3
Eggs 3
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Toa karanga maganda na zisage kwa kutumia blenda ya vitu vikavu
Peel the Groundnuts and crush them by using food processor
2.Katika bakuli weka siagi na sukari
Mix butter and sugar in a bowl
3.Saga kwa dakika kadhaa mpaka ichanganyike
Use hand mixer to beat the mixture till mixed
4.Weka baking powder saga kwa dakika 1
Add baking powder and keep mixing for 1 minutes
5.Weka arki endelea kusaga kwa dakika 1
Add Pine Apple Essence and beat for another 1 minutes
6.Saga kwa dakika kadhaa mpaka ichanganyike vizuri na sukari ipotee
Use hand mixer to beat the mixture until they are light and fluffy
7.Weka vijiko viwili vikubwa vya karanga zilizosagwa kwenye mchanganyiko wako kisha saga kidogo
Add two table spoon of crushed groundnuts in the butter mixture and keep beating for 1 minutes
8.Weka mayai mawili endelea kusaga kwa dakika moja
Add two eggs and keep beating the mixture
9.Kisha weka unga wa ngano uliochekechwa mpaka ushikane na kuwa donge laini ukishikana tu basi
Add the sifted plain flour till you get a very soft dough
10.Chukua trea weka karatasi za kuokea au karatasi nyeupe yoyote
In a baking tray add the baking paper
11.Kata donge dogo weka mkononi lifanye liwe na umbo la mpira
Take small dough then shape the dough as a ball by using your hand
12.Kisha chini lifanye bapa na juu liwe duara vile vile
Then flatten the ball at the bottom and at leave the upper side into a ball shape
13.Bonyeza kati kati ya kileja upate kishimo kidogo
Press the center to get a small hole
14.Chukua jam weka kwenye kishimo
Add the jam in the hole
15.Piga yai lako kisha vipakae vileja vyote vizuri
Beat an egg and apply it on the upper side of your cookies
16.Chukua kileja weka mkononi kinyunyizie karanga zilosagwa
Take a cookie and sprinkle the crushed ground nuts on top
17.Washa jiko la kuokea(Oven/Cooker) moto wa 170
Pre heat or heat the Oven around 170'C
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka Butter balls acha ziive kwa dakika 20 tu
Bake the Butter Balls for 20 minutes only
2.Zitoe ndani ya jiko utaziona laini kidogo acha zipoe humo humo kwenye trei
Remove from the oven let them cool while they are in the tray
3.Acha zipoe kama dakika 5 mpaka 10
Let them cool for 5 to 10 minutes
4.Tayari kula na kinywaji upendacho au zenyewe
You can serve with any drink you prefer
Angalizo:Note;
1.Hakikisha unasaga hadi sukari inapotea
Make sure you beat the mixture till light and fluffy
2.Usitengeze pana sana kwani huumuka wakati wa kuzioka
Make sure the cookies height is not wider since it raises during baking
3.Wacha nafasi baina ya butter balls moja na nyengine zikiwa jikoni hutanuka zikipata moto
Leave enough space between one Butter Balls and another in the baking tray because they expand when heated
4.Usifanye shimo kubwa la jam kila inapopata moto nalo huongezeka ukubwa
Don't create a large hole at the center of Butter Balls it may increase in size when heated
5.Kama jiko lako lina moto mkali basi hakikisha zikibadilika rangi na kuonekana ngumu kidogo zitoe
If you can not control the temperature of the your oven remove the Butter Balls into the oven once you see the upper side turns into light golden brown colour
6.Usitoe kwenye trei kama hazijapoa zinaweza kuvunjika
If they are not cool yet don't remove them from the baking tray they can break since they are not cool
7.Hakikisha hauzisagi karanga mpaka zikawa unga
Do not crush(mush) the ground nuts until powdered
8.Hakikisha una paka yai vizuri ili karanga ziweze kuganda
Make sure you apply the beaten egg well enough to let the ground nuts stay on the Butter balls
9.Unaweza kuweka zabibu nyeusi katikati badala ya jam
You can keep black raisin at the center instead of jam
Furahia Butter Balls Zako.
2 comments:
Salaam alaykum,
Hongera sana kwa mapishi mazuri ila kama sina rice cooker cup naweza tumia kikombe gani?
Waalaikum Salaam tumia kikombe kidogo cha chai
Chapisha Maoni