MAHITAJI
1.Viazi Mbatata
Robo(1/4 kg)
2.Mafuta ya kula nusu
lita
3.Mayai yaliyo chemshwa
6
4.Chumvi kiasi
5.Juisi ya Ndimu kijiko
kikubwa 1
6.Pilipili ilosagwa
Nusu kijiko cha chai
7.Mayai mabichi 3
8.Unga wa mchele au wa
Sembe Vijiko vya Chakula 3
9.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Menya viazi mbatata
kata vipande kiasi
2.Osha viazi weka maji
na chumvi kiasi
3.Vunja mayai weka
chumvi
4.Yapige mayai kisha
weka pembeni
5.Menya mayai yalio
chemshwa weka pembeni
JINSI YA KUPIKA
1.Chukua sufuria
ulioweka mbatata acha ichemke mpaka viazi viwe laini na kuiva.
2.Kisha vimwage maji
virudishe jikoni vikauke kwa dakika 1tu.
3.Epua viazi viponde
kwa mwiko wa ugali mpaka vipondeke
4.Chukua viazi
vilopondwa kiasi weka kwenye mkono tengeneza shimo la kuingia yai
lilochemshwa
5.Weka yai kati kati ya
shimo la viazi kisha weka sawa viazi kuficha lile yai
6.Rudia kwa mayai yote
yalobakia
7.Nyunyizia unga kwenye
maduara ya katlesi zako
8.Chukua karai mimina
mafuta wacha yapate moto sana hadi yatoe moshi
9.Tumbukiza katlesi
kwenye mayai mabichi kisha weka kwenye mafuta yamoto
10.Iache bila kuigusa
kwa dakika 3 mpaka iwe ya brown
11.Igeuze kisha acha
kwa dakika 3 nyengine toa chuja mafuta.
12.Inaweza kuliwa
yenyewe au na chapati au mkate wowote
Angalizo:
1.Viazi usiviponde kama havijakauka vizuri vikiwa vya maji vitafanya maji ndani baada ya kuiva
2.Usiweke katlesi kama mafuta hayajapata moto vizuri
2.Usiweke katlesi kama mafuta hayajapata moto vizuri
3.Hakikisha katlesi
imezama kabisa kwenye mafuta la sivyo itapasuka kwenye karai
4.Unaweza kuweka bread crumbs ukikosa unga wa mchele
5.Usiweke unga wa ngano kama mbadala wa unga wa sembe
6.Mayai yachemshwe na chumvi kiasi
4.Unaweza kuweka bread crumbs ukikosa unga wa mchele
5.Usiweke unga wa ngano kama mbadala wa unga wa sembe
6.Mayai yachemshwe na chumvi kiasi
Furahia Katlesi Zako.
3 comments:
hii juici ya ndimu inatiwa wakati gani
somo zuri hata mm kesho wageni wangu nawaandalia kwenye break te#chefsaifary
Some zuri saana
Chapisha Maoni