Jumatano, 1 Juni 2016

CHAI YA VIUNGO(SPICED TEA)

MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Maji Lita 1
  1 Litre Water

2.Mdalasini mzima Vipande vikubwa 2
  2 Stick Cinnamon

3.Majani ya Chai kijiko cha chakula 1
  1 Tbsp Tea Leaves
 
4.Hiliki punje 5
 5 Cardamon Cloves
 
5.Tangawizi ilioparwa kijiko cha chakula 1
 1 Tbsp Grated Ginger

6.Sukari nusu kikombe cha Chai
 1/2 Cup Sugar

MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Mimina maji kwenye sufuria
 Pour some water on a big pan or pot

2.Twanga hiliki na sukari kiduchu
 Mix the seed of cardamon with a pinch of sugar and grind them to get cardamon powder

3.Weka Tangawizi,hiliki na mdalasini kwenye maji
 Add ginger,cardamon powder and cinnamon stick in a pan added water

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka sufuria jikoni wacha maji yachemke sana
 Bring water to a full boil
 
2.Baada ya kuchemka vizuri weka majani na sukari
 Then add tea leaves and sugar
 
3.Acha yachemke kidogo kama dakika 3 epua
 Let it boil for 3 minutes more
 
4.Mimina kwenye chupa tumia kichujio kuchuja viungo na majani ya chai
 Pour the tea in a thermo use small sieve to filter the spice and tea leaves
 
5.Unaweza kunywa na kitafunio chochote kama chapati,keki,andazi n.k
 You Can serve with Bread,cake,cookies etc

Angalizo:Note
1.Usiweke majani kama maji hayajapata moto vizuri hubadilisha ladha ya chai
 Dont add tea leaves if the water is not well boiled

2.Kama unapenda sukari nyingi unaweza weka zaidi ya hio hapo juu
 You can add more sugar if you like too much sugar in a tea

3.Usiweke majani ya chai mengi husababisha chai kuwa chungu
  Adding too much tea leaves lead the tea to become bitter

4.Usiache Chai Ichemke Muda mrefu baada ya kuweka majani
  Dont over boil after adding tea leaves

 
Furahia Chai Yako.

0 comments:

Chapisha Maoni