Jumatano, 18 Mei 2016

SHRIMPS RICE(WALI WA KAMBA)


MAHITAJI/INGREDIENTS

1.Kamba wakubwa kiasi 30
 30 Medium size shrimps

2.Mchele Kikombe Kimoja
 1 Cup uncooked rice

3.Keroti kubwa 1
 1 Carrot

4.Pilipili Boga kubwa 1
 1 Medium size Green Pepper

5.Kitunguu kikubwa 1
  1 Medium size Onion

6.Ndimu ilokamuliwa kijiko 1
 1 Tbsp Lemon juice

7.Pilipili inayowasha 1
 1 Red Chilli

8.Kitunguu punje kubwa 1
 1 Garlic Clove

9.Chumvi kiasi
 Salt to taste

10.Fish Masala kijiko kidogo 1
 1 Tea spoon Fish Masala

11.Mafuta robo kikombe
 1/4 Sun Flower Oil

12.Tangawizi Ndogo sana
 1 small Piece Fresh Ginger

13.Uzile(Binzari Nyembamba) kijiko cha chai 1
  1 Cumin seeds Tea spoon

14.Nyanya(Tungule) 1
  1 Fresh Tomato

MAANDALIZI/PREPARATION

1.Chukua kamba waoshe vizuri kisha watoe magamba yao yote
  Wash well the shrimps and peel them well

2.Menya Kitunguu thomu na tangawizi
   Peel the ginger and clove of garlic then wash them

3.Twanga kitunguuu thomu,tangawizi,pilipili na chumvi kwa kutumia mchi na kinu
 Grind the mixture of ginger,red chilli,salt and clove of garlic I do use (mortar and pestle)

3.Waweke kwenye bakuli dogo na waunge vizuri kwa kuwaweka viungo ulivyovisaga
  Marinate them by adding the mixture you grind in step 2

4.Weka Ndimu,Masala na Uzile kisha wachanganye vizuri 
  Finally add Masala,Lemon juice and cumin seed then mix them well

5.Chambua mchele na uoshe vizuri weka pembeni
 Remove the unwanted particle in rice and wash it well

6. Para keroti kisha kata vipande vikubwa kiasi vya Kitunguu maji 
  Grate the Carrots and by using sharp knife chop the onion into medium size

7. Toa mbegu za kati za Pilipili hoho kisha ikate vipande kwa urefu
     Remove the inner seeds and chop it into little sticks

8.Para nyanya weka pembeni
  Grate the tomato and set a side

9.Weka maji kwenye sufuria na chumvi 
  Add water and salt into pot

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK

1.Weka maji jikoni yakipata moto pika wali mpaka uive
  Bring the water to a full boil and cook the rice until cooked

2.Weka karai na mafuta yakichemka kaanga kitunguu mpaka kiwe brown kiasi
  Add the oil into the pan and when heat fry the onion till light brown

3.Weka pillipili hoho kaanga kidogo mpaka zitoe harufu tu usikaange sana kama kitunguu maji
 Add the green pepper fry till smell dont over cook like onion

4.Malizia keroti nazo ziache kidogo tu
  Add grated carrot and keep frying

5.Weka wale kamba na koroga mpaka wabadilike rangi na kuwa na rangi ya dhahabu
    Add marinated shrimps and steer the mixture till the shrimps turn to golden colour

6.Malizia kuweka nyanya na chumvi kidogo sana
 Finaly add grated tomato and a pinch of salt

6.Koroga acha kwa dakika 1
 Steer the mixture and leave it for 1 minute

7.Mimina wali ulio upika mwanzo kwenye mchanganyiko wa kamba
  Add the cooked rice in the shrimps mixture

8.Uchanganye kisha ufunike uache ukauke kwa kiasi cha dakika 5
  Mix well and cover it to get dried for 5 minutes

9.Baada ya muda huo pakua unapendeza kuliwa na juice au soda.
  When its ready you you can serve with juice or soda

Angalizo:Note
1.Usiweke mafuta mengi wakati wa kukaanda
 Do not add too much oil when frying

2.Usiongeze pilipili unaweza kuwasha watoto wakashindwa kula
 Dont add too much chilli pepper

3.Unawasha kwa mbali kama hupendi chakula kinacho washa usiweke pilipili
  Dont add chilli if you dont like too much chilli in your food 

Furahia Wali Wako.
  

0 comments:

Chapisha Maoni