Pages

Pages - Menu

Alhamisi, 5 Mei 2016

WALI WA KUKU WA MVUKE



MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Mchele wa Basmat Robo(1/4 kg)
 1/4 kg Basmat Rice

2.Mafuta ya kula robo lita
  1/4 litre Cooking Oil

3.Kitunguu maji kikubwa 1
 1 Medium Size Onion

4.Karoti kubwa 1
 1 Large Carrot

5.Pilipili Hoho(Pilipili boga) kubwa 1
 1 Large Green Pepper

6.Chumvi vijiko vikubwa 3
 3 Tbsp Salt

7.Uzile mzima(Binzari Nyembamba) kijiko Kikubwa 1
 1 Tbsp Cumin(cummin) seeds

8.Kitunguu thomu kilosagwa kijiko kikubwa 1
 1 Tbsp Minced Garlic

9.Tangawizi ilosagwa vijiko vikubwa 2
  2 Tbsp Crushed Ginger

10.Juisi ya Ndimu vijiko vikubwa 2
 2 Tbsp Lemon Juice 

11.Viazi Mbatata vidogo 8
 8 Small size Potatoes
12.Chicken Masala vijiko 2
 2 Tbsp Chicken Masala

13.Maji kiasi
 Water for boiling rice

14.Kuku Nusu
1/2 Chicken

15.Rangi ya Zafarani(Sio Lazima)
Zafarani(Orange Colour) Option

16.Njegere robo kikombe
1/4 Cup Peas


MAANDALIZI/PREPARATION
1.Osha mchele wako vizuri uweke pembeni
  Rinse the Basmat rice well

2.Katakata kitunguu maji,karoti na pilipili kila kimoja kata kwenye sehemu yake usivichanganye
 Chop the Onion,carrot,green pepper separately dont mix them after chopping 

3.Menya viazi mbatata kisha kata kata kwa umbo la chipsi.
 Peel the Potatoes and cut them in chips shape

4.Kata kata kuku vipande kisha muoshe vizuri
 Cut the chicken into pieces and wash them well

5.Muweke Kuku wako Chumvi kijiko 1,ndimu,tangawizi,kitunguu thomu na chicken masala na muwache kwa robo saa katika friji
Marinate the chicken with salt,lemon juice,ginger,garlic and chicken masala then refrigerate it for at least quarter an hour

6.Chukua kikombe weka maji kiduchu na rangi kiasi
 Put the orange colour and some drops of water in a cup


JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Chukua sufuria weka maji,chumvi kijiko 1,njegere na uzile yakichemka toa uzile wako wote na kisha weka mchele acha uchemke na uive kisha umwage maji uache bila maji.
Add water,1 tsp of salt and cumin seed in a cooking pot and bring to full boil then remove all cumin seeds and add the rice and let it boil till cooked,strain the rice in sieve or colander.

2.Chukua sufuria weka maji funika na chujio la rice cooker na umpange kuku wako halafu funika na foil mpike kwa dakika 15 .Hakikisha humwagi rojo rojo lilobakia kwenye kuku utakuja kuyatumia baadae
In another pot add some water cover the pot with rice cooker steamer,place the chicken on rice cooker steamer then cover it with foil and the lemon juice remained in the chicken bowl during marination leave it for further uses,let it cooked for 15 minutes while it is on the stove.

3.Baada ya dakika kupita mgeuze kuku na muwache tena kwa dakika 15
 After those minutes turn over the chicken so can be cooked in another side

4.Akiiva mtoe weka pembeni
 When it is ready remove from the steamer to the plate

5.Chukua sufuria nyengine uweke mafuta na kaanga chipsi mpaka ziive kisha zitoe
 In another pot add the Oil and Fry the chips till cooked and keep it a side

6.Ukitoa chipsi anza kukaanga vitunguu maji mpaka viwe brown kiasi kisha vitoe,halafu kaanga keroti na uzitoe na malizia kukaanga pilipili boga na kisha zitoe
 Then fry the onion till brown when ready keep it aside,then fry carrot then remove it and finally fry the green pepper and remove it dont mix them

7.Chukua chombo yatoe yale mafuta yote uliokaangia na bakisha sufuria tupu
 Remove all the cooking oil in a pot

8.Mimina wali uliopika kwenye ile sufuria kidogo kisha juu weka viazi mbatata,kisha ongeza wali kidogo juu ya viazi mbatata kisha weka kuku
In an empty pot make layer of rice with vegetable by starting add cooked rice little then add chips on top of rice than rice again then steamed chicken

9.Endelea kwa kuweka pilipili boga ulilolikaanga kisha mimina wali ,nyunyizia chumvi juu weka vitunguu maji na rudia hivyo hivyo mpaka mwisho juu kabisa weka rangi.
Continue to add fried green peppers than rice on top than spread some salt then fried onion then salt and add the colour on top of rice 

10.Mimina lile rojo rojo la kuku uliloli bakisha kisha ufunike wali wako upate kukauka
 Add the lemon juice remained in the chicken bowl during marination on top of the rice

11.Acha wali ukauke kwa moto mdogo kwa dakika 5 usiukoroge.
 Cover the rice for 5 minutes with medium heat

12.Baada ya huo muda kupita uepue kisha uchanganye na upakue
 After that time passes you can serve it


Angalizo:Note
1.Pangilia vizuri wali kwa kutenganisha na viungo pamoja na kuku
 Make sure you make the layer between rice and chicken with fried vegetables

2.Sio lazima upange kama nilivyo orodhesha hapo juu ila ni muhimu kutenganisha viungo na wali wako
 You can make the layer as you wish not necessary to follow how i did

3.Usiukoroge mpaka wakati wa kuupakua
 Dont mix the rice till when it is ready to serve

4.Unaweza kuweka mbogamboga zaidi
 You can add more vegetables you have


Furahia Wali Wako.


Maoni 2 :