MAHITAJI
1.Viazi vitamu
vikubwa 5
2.Nazi pakti 1
3.Sukari vijiko vha
chakula 5
4.Arki Vanilla
kijiko cha chai 1
5.Custard kijiko cha
chakula 1
9.Hiliki punje 10
10.Chumvi kijiko cha
chai 1
11.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Menya viazi na
uvikate vipande vidogo vidogo
2.Vioshe na uviweke
kwenye sufuria safi na maji kiasi
4.Menya na utwange
hiliki
5.Chukua tui gawa
sehemu mbili.Robo weka kwenye kikombe lilobakia weka kando
6.Chukua tui robo
kikombe weka custard na ikoroge vizuri
JINSI YAKUPIKA
1.Chukua chumvi weka
kwenye viazi vyako weka jikoni acha vichemke hadi viive
2.Mwaga maji
yaliyobaki acha viazi vilivyo iva bila ya maji
3.Weka tui
lililobaki kwenye viazi viloiva pamoja na sukari na hiliki na
urudishe jikoni kwa moto wa wastani
4.Acha vichemke kwa
dakika 5 hadi tui lipungue
5.Malizia kwa kuweka
arki na tui lenye custard
6.Acha dakika 1
jikoni na viepue
7.Acha vipoe pakua
tayari kwa kula
8.Inapendeza kula na samaki wa kukaanga
Angalizo:
1.Usiviache
vikachemka hadi vikavurugika kabla ya kuweka tui
2.Usikoroge mpaka
wakati wa kuvipakua
3.Unaweza kupika na
nazi ya kawaida au ya unga
4.Sio lazima kuweka
custard
Furahia Viazi
Vitamu Vyako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni