Pages

Pages - Menu

Ijumaa, 25 Desemba 2015

CHAPATI ZA MAJI(PANCAKES)


MAHITAJI/INGREDIENTS

1.Unga wa ngano nusu kilo
 1/2 kilogram of All Purpose flour

2.Kitunguu maji kikubwa 1
 1 big Onion

3.Pilipili boga 1
 1 Green pepper

4.Karoti 1
 1 Carrot

5.Yai 1
 1 Egg

6.Chumvi cha chakula 1
 1 Tbsp of Salt

7.Mafuta nusu kikombe
 1/2 cup of Cooking oil

8.Maji kikombe kikubwa 1 au zaidi
 1 Big Cup of water or more

9.Sukari kijiko cha chai kimoja 1
 1/2 Tbsp of sugar


MAANDALIZI/PREPARATION
1.Chukua bakuli kubwa kiasi chekecha unga weka pembeni
 Sift the flour in a big bowl and keep it a side.

2.Kata kata vitunguu maji kama vya mchuzi vifikiche kwa mkono kuviachanisha weka pembeni
 Cut the onion in small sized pieces and crumble them by your hand

3.Para karoti weka pembeni
 Grate the carrots

4.Kata pilipili boga nyembamba weka pembeni
 Cut thin and small pieces of  green pepper

5.Vunja yai kwenye kibakuli lipige na umma kama unataka kulikaanga weka pembeni
 Take a small bowl and folk then beat an egg keep it a side

6.Chukua maji weka kidogo kidogo kwenye unga huku ukiuchanganya na mchapo au upawa mpaka uwe na uzito kiasi hakikisha hauwi mwepesi sana wala mzito sana
 Pour water slowly in a flour and mix it well then whisk the wet mixture and make it neither heavy nor light

7.Mimina vitunguu,karoti na pilipili boga kisha koroga uchanganye vizuri
Put onion,carrots and green pepper in your wet mixture and whisk it 

8.Weka chumvi ,sukari na yai kisha changanya vizuri mpaka uji wako uchanganyike na vitu vyote
 Put salt,sugar and bitten egg and keep whisk the mixture till all ingredient well mixed

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka chuma(frying pan) chako jikoni na mafuta kijiko kimoja yaeneze kwenye chuma chote
 Pour a Tbsp of oil in Non Stick Frying Pan and swirl around so that it lightly coats the surface,let it heated for a minute

2.Tumia upawa chota miko miwili au zaidi inategemea na ukubwa wa chuma chako na ieneze kwenye chuma chote
Use a cooking spoon mix well your wet mixture then take two of them and pour the mixture in a frying pan

3.Acha kwa dakika 3 mpaka uone mkate wote umekauka ile umaji maji wa ubichi haupo
  Let cooked for 3 minutes till the upper side become dry

4.Ugeuze upande wa pili uache pia kwa dakika 3 ukauke
 Carefully lift the edge of the pancake with spatula and flip on the another side and cook again till dried for about 3 minutes

5.Chota mafuta kijiko kimoja weka chini ya mkate wako huku ukiuzungusha mpaka upate yangi ya kuvutia
 Put a Tbsp of oil at bottom of your cooked pancake and use a Tbsp to squeeze it till have golden brown colour

6.Ugeuze kisha utoe weka kwenye kwenye sahani
 Flip over and and remove it from pan to the plate

7.Rudia njia hizi mpaka umalize uji wote
Repeat the above procedure till you finish the whole wet mixture

8.Weka mezani kula na chai ya maziwa,juice au kinywaji chochote
 Serve with tea,milk,juice or any drink

Angalizo:Note
1.Yai muhimu usipoweka mikate inaganda kwenye chuma
 You must put an egg otherwise the pancake will sticky in pan 

2.Kama utakosa yai weka mafuta kijiko 1 cha chakula
 Use a Tbsp of cooking oil in absence of an egg

3.Tumia Nonstick Frying Pan kwa kuhofia kugandisha mikate mara kwa mara
 Use Nonstick Frying pan to avoid sticking of pancakes frequently

4.Ili upate mikate mizuri ya kuvutia hakikisha moto ni wa wastani ukipikia moto mkubwa zinakua mbaya
 Use medium heat to get delicious and attractive pancakes otherwisewont have good taste

Furahia Chapati Zako.

Maoni 5 :