skip to main |
skip to sidebar
MAHITAJI
1.Mchele wa basmat nusu kilo
2.Karoti kubwa 1
3.Pilipili boga(Pilipili hoho) kubwa 1
4.Kitunguu maji kikubwa 1
5.Mafuta kiasi
6.Chumvi kiasi
7.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Osha mchele wako kisha uweke maji kiasi
2.Loweka mchele kwa nusu saa
3.Para karoti yako weka pembeni
4.Kata kata vitunguu maji na pilipili hoho weka pembeni
JINSI YA KUPIKA
1.Weka kikaangio jikoni kisha tia mafuta
2.Anza kukaanga vitunguu maji kisha pilipili boga na malizia karoti
3.Usivikaange sana mpaka vikawa brown kama vya mchuzi
4.Toa viungo vyako weka kwenye kibakuli na mafuta yake
5.Chukua sufuria ya kupikia wali mimina maji ulio rowekea mchele
6.Yaweke chumvi na weka jikoni yapate moto
7.Acha yachemke kisha weka mchele na uache uive
8.Acha maji yakauke kidogo mimina vitu ulivyo vikaanga na mafuta yake kwenye wali wako
9.Acha ukauke na uive vizuri
10.Pambia ila hakikisha haufanyi matandu
11.Pakua tayari kwa kula na kitu chochote upendacho
NB: 1.Hakikisha viungo havikaangwi sana
2.Usiache wali ukauke kabisa kabisa ndio uviweke viungo
3.Usiongeze mafuta zaidi uliyo kaangia kwenye wali
Furahia Wali Wako
MAHITAJI
1.Tambi za spaghettini pakti 1
2.Kuku nusu
3.Nyanya (Tungule) kubwa 3
4.Pilipili hoho(pilipili boga) 1
5.Karoti kubwa 1
6.Mafuta kiasi
7.Tangawizi iloswagwa kijiko cha chakula 1
8.Kitunguu thomu kilosagwa kijiko 1
9.Royco(Ukipenda) kijiko 1
10.Chumvi kiasi
11.Kitunguu maji
12.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Kata kata vipande vyako vya kuku upendavyo
2.Muoshe kisha muweke pembeni
3.Kata kata Pilipili hoho na keroti kwa umbo la pembe nne(square)
4.Kata kata vitunguu maji weka pembeni
5.Para au saga nyanya zako weka pembeni
6.Vunja tambi zako weka pembeni
JINSI YA KUPIKA
1.Muweke kuku wako tangawizi,kitunguu thomu na chumvi
2.Kisha muweke jikoni mwache kidogo kisha weka maji
3.Chemsha kuku wako mpaka aive
4.Weka maji jikoni mpaka yachemke kidogo
5.Weka tambi zako zikiiva zichuje maji ziweke pembeni
6.Weka sufuria kavu na weka mafuta kwa ajili ya kukaanga
7.Anza kukaanga vitunguu maji kisha pilipili hoho na malizia na karoti
8.Weka nyanya acha dakika 1 kisha weka chumvi kiasi
9.Mimina nyama yako ya kuku koroga acha dakika 2 kisha onja kama chumvi ipo sawa malizia kwa kuweka tambi
10.Changanya tambi vizuri subiri kidogo zikauke ule mchuzi ubaki kidogo sana
Angalizo:
1.Hakikisha tambi huzichemshi mpaka zikavurugika
2.Usimimine tambi kama mchuzi haujapungua
3.Usikaushe tambi zako kabisa kabisa acha zikiwa na rosti kwa mbali
Furahia Tambi Zako.
MAHITAJI
1.Samaki umpendae
2.Pilipili ya kuwasha 1
3.Vitunguu thomu punje2
4.Chumvi kiasi
5.Ndimu 1 kubwa
6.Mafuta kikombe kikubwa 1
7.Unga wa sembe robo
8.Maji kiasi
MAANDALIZI
1.Osha Samaki wako baada ya kumpara na kuondoa Maganda yote
2.Mkate Kate au mpasue tu ili aweze kuingia Viungo vizuri
3.Twanga Pilipili, Kitunguu thomu na Chumvi kisha weka kwenye Samaki wako
4.Mkamulie Ndimu kisha muache kwa dakika 30 au zaidi ako lees Viungo ukipenda muweke kwenye fridge
5.Chunga Unga wako wa ugali weka pembeni
6.Weka maji kiasi kwenye sufuria ndogo unayo taka kusongea ugali wako
7.Chukua kibakuli weka maji kisha chota Unga miko miwili na ukoroge kama unataka kupika uji
JINSI YA KUPIKA UGALI
1.Weka maji jikoni acha yapate moto kidogo
2.Mimina uji ulioukoroga pembeni kwenye sufuria yako
3.Koroga hakikisha uji sio mwepesi sana wala mzito sana
4.Acha uchemke mpaka utokote kisha anza kuweka Unga mkavu kidogo kidogo huku ukiukoroga
5.Songa ugali wako kwa dakika 4 kisha acha kidogo utulie
6.Endelea kuusonga tena mpaka uwe mlaini kwa dakika 5
7.Ufunike kidogo kwa dakika moja kisha pakua
8.Weka kwenye sahani au hot pot
9.Kula na Samaki, kachumbari, Maharage, Mchuzi, Nyama 'n.k.
JINSI YA KUPIKA SAMAKI
Kuna njia mbili: Unaweza kumkaanga au kumchoma
1.Kukaanga weka frying pan au karai jikoni weka mafuta
2.Yakipata moto muweke samaki wako
3.Baada ya dakika 4 mgeuze upande wa pili
4.Muwache aive upande mwengine kisha mtoe
5.Muweke kwenye tissue au chujio achuje mafuta
6.Akipoa tayari kwa kula
7.Hakikisha moto ni wa wastani usiwe mdogo wala mkubwa
8.Usiweke samaki kwenye mafuta mpaka yapate moto kisawa sawa
Ama kwa kumchoma
1.Chukua wavu wa kuchomea samaki au nyama
2.Weka samaki wako mwache kwa dakika 1 kisha mpake mafuta
3.Hakikisha moto ni mdogo kiasi ili asiungue
4.Baada ya dakika 5 mgeuze upande wa pili na mpake tena mafuta
5.Msubiri kwa dakika 5 nyengine kama kaiva mtoe
NB: 1.Ili ugali uwive hakikisha maji yanachemka vizuri
2.Jitahidi kuusonga vizuri ili uwe mlaini
3.Tumia mwiko wa ugali kusongea ugali
Furahia Ugali na Samaki Wako.
MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Viazi mbatata nusu(Vyenye Ngozi Ya Brown)
1/2 Kg Potatoes(Russets)
2.Samaki 4(Vibua)
4 Fish(Razor Bellies fish)
3.Mafuta ya kupikia litre 1
1 Litre Cooking Oil
4.Mayai 4
4 Eggs
5.Keroti Kubwa 1
1 Large Carrots
6.Ndimu 4
4 Lemon
7.Kitunguu thomu punje kubwa 6
6 Garlic Cloves
8.Chumvi kiasi
Salt to taste
9.Tangawizi ndogo 1
1 Small Ginger
10.Pilipili ya kuwasha 2
2 Red Chillies
11.Paprika kijiko cha chakula 1
1 Tbsp Paprika
12.Unga wa mchele (Unga wa sembe au Bread crumbs)
Rice Flour or Bread Crumbs
13.Maji
Water
14.Royco Paketi 1
1 Packet Royco
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Osha Samaki muweke pembeni
Wash the fishes well and put them in the cooking pot
2.Menya Viazi na vikate Kate weka pembeni acha na maji
Peel the potatoes and cut into small pieces wash them,keep the pieces in another cooking pot with water
3.Osha vitu vilobakia
Wash other ingredients remain
4.Menya Tangawizi na Kitunguu thomu kisha vitwange na pilipili usiweke Chumvi
Peel the ginger and garlic cloves and mix with chillies then grind them together without salt
5. Vunja Mayai weka kwenye kibakuli na Chumvi kidogo yapige kama unataka kukaanga kisha weka pembeni
Break the eggs in the bowl add salt then beat them
6. Chukua kibakuli na ukamue Ndimu na maji kidogo na ziweke pembeni
In another separate bowl squeeze the lemon with little water and keep them aside
7.Para keroti yako weka pembeni
Grate the carrots keep it aside
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1. Chemsha Samaki wako na Chumvi na Ndimu pamoja na Royco hakikisha haumkaushi anabaki na maji maji
Add the lemon juice,salt and royco in the pot of fishes and bring it to boil until cooked but leave the fishes with little amount of water
2. Chemsha Viazi mbatata na Chumvi kiasi acha vichemke kisha vikiiva mwaga maji na rudisha jikoni kwa dakika 1 ili viwe vikavu kisha epua
Bring to boil the pot of potatoes add salt and when they are ready drain them and take the pot back to the stove for some seconds let the potatoes dry completely
3. Mtoe Samaki miba chukua nyama yake iweke Pilipili ulioitwanga changanya vizuri kisha weka pembeni
Remove the bones and pin bones of the boiled fish and take the fillet into the bowl add the chillies mixture and mix it well and keep it aside
4. Chukua mwiko wa ugali au chupa ponda ponda vile Viazi ulivyo vichemsha mpaka vilainike vyote
Mash the boiled potatoes very well
5. Changanya Samaki,Viazi ulivyo viponda na keroti vizuri
Mix the mashed potatoes with fish mixture and grated carrots by spatula or hands
6. Chukua donge la Viazi tengeza shape upendayo kisha nyunyizia Unga wa mchele kidogo juu ya katlesi zako
Take small portion of mashed potatoes mixture then shape into any shape you desire keep into the plate then sprinkle the flour or bread crumbs on top
7. Weka mafuta jikon hakikisha yamekuwa ya moto sana chovya katlesi kwenye Mayai kisha weka kwenye karai
Pour the oil into frying pan and let it heat to the maximum and insert the cutlets beaten eggs then put it in the frying pan
8. Acha kwa dakika 3 kisha zigeuze acha dakika kadhaa zikiwa na rangi ya dhahabu zitoe
Leave them for 3 minutes then flip to let the other side to cook evenly when turn into golden brown remove from the pan
9. Weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta zikipoa tayari kwa kula
Remove from the pan to the sieve or tissue to get dried
10. Unaweza kula zenyewe au kwa chapati au na urojo
You can serve with breads,urojo or as they are
Angalizo:Note;
1. Usiharakize kuzipika kabla mafuta hayajapata moto zitapasuka kwenye karai
Do not hurry to insert them into the oil before is heated enough they will break in the frying pan
2. Kaangia kwa Mayai ya kutosha ili zipendeze
Use enough beaten eggs to be covered well and have better skin
3. Usiwe na haraka ya kuzitoa jikoni acha ziive ndio uzigeuze au uzitoe
Do not flip or remove from the frying pan if they are not ready
4.Ukikosa vibua tumia samaki wa vipande hasa nguru
You can use King Fish instead of Razor Bellies Fish
5.Tumia viazi mbatata vya brown huwa vikavu na rahisi kuviponda ponda
Use Russets potatoes or Yukon Gold Potatoes since they are can be mashed easily
6.Kupata ladha tamu na nzuri ya Katlesi ni vizuri kula zikiwa zimepoa
Let the cutlets cool before you serve them
Furahia Katlesi Zako
MAHITAJI
1.Unga wa ngano nusu kilo
2.Mtindi wa ml 750
3.Chumvi kijiko cha chakula 1na nusu
4.Sukari nusu kijiko cha chakula
5.Samli kikombe kidogo cha chai nusu
6.Mafuta ya kupikia nusu kikombe
7.Maganda ya Chungwa kijiko cha chakula 1
8.Juice ya chungwa vijiko 4
9.Maziwa ya unga robo kikombe
10.Ute wa mayai 2
11.Kungu manga(sio lazima)
MAANDALIZI
1.Chunga unga wako weka kwenye chombo cha kukandia
2.Weka chumvi,maziwa,maganda ya machungwa changanya weka pembeni
3.Chukua mtindi,weka sukari na juice ya chungwa piga piga na umma mpaka uchanganyike vizuri
4.Tia ute wa yai kwenye unga wako changanya na mwiko unga wako vizuri
5.Weka mtindi kwenye unga wako na uchanganye vizuri kisha ukande kwa dakika 5 mpaka ulainike
6.Funika unga wako kwa dakika 10 kisha uweke samli vijiko 3 endelea kuukanda mpaka uwe unavutika kwa dakika 10
7.Kisha funika tena kwenye container kwa muda wa nusu saa
8.Katakata madonge kulingana na size ya chapati unayoitaka
9.Sukuma madonge yako duara kisha yapake samli kati na sokota na uyapange kwenye bakuli lenye mfuniko na uyaache kwa nusu saa
10.Baada ya hapo utaanza kusukuma duara kwa ajili ya kupika chapati
JINSI YA KUPIKA
1.Yeyusha samli ilobaki changanya na mafuta
2.Weka kikaangio chako jikoni hakikisha moto ni wa wastani
3.Weka chapati yako mpaka ifanye brown
4.Geuza Chapati yako upande wa pili ikiwa ya brown weka mafuta kijiko kimoja
5.Izungushe chapati yako huku ukiikandamiza na kijiko ili kuilainisha kati mpaka nchani
6.Toa chapati weka nyengine mpaka umalize chapati zako
NB:
1.Ili chapati ziwe laini hakikisha unakanda kwa muda mrefu mpaka zinalainika
2.Ipe mda wa kutulia kabla kuipika
3.Usipende kuiweka mafuta mengi wakati wa kupika
4.Usigeuze geuze mara kwa mara wakati wa kuchoma
Furahia Chapati Zako.
MAHITAJI
1.Ndizi mbichi
2.Nyama robo
3.Nyanya kubwa(Tungule) 4
4.Nazi moja kubwa
5.Ndimu 1
6.Karoti 1
7.Pilipili Hoho(Pilipili boga)1
8.Kitunguu maji kikubwa 1
9.Kitunguu thomu punje 3
10.Nyanya ya Paket vijiko vya chakula 2
11.Royco(Sio lazima)
12.Tangawizi na kitunguu thomu ilotwangwa kijiko cha chakula 1
MAANDALIZI
1.Osha viungo vyako vyote vinavyotakiwa kuoshwa
2.Katakata Nyanya,Kitunguu maji,thomu,Pilipili hoho weka kwenye blenda na uvisage vyote
3.Kuna nazi yako na ichuje
4.Weka tui zito na jepesi mbalimbali
JINSI YA KUPIKA
1.Chemsha nyama uloiweka tangawizi kitunguu thomu na chumvi mpaka iwive
2.Chemsha ndizi weka pembeni
3.Weka nyanya ulizozisaga kwenye nyama yako acha ziive
5.Weka nyanya ya paketi na Royco
6.Weka chumvi na ndimu kama imepungua ongeza chumvi kidogo
7.Weka tui jepesi kwenye ndizi na chumvi acha zichemke kwa dakika 3 usikoroge
8.Kisha weka tui zito acha lichemke kwa dakika 2
9.Weka mchuzi wako wa nyama acha kwa dakika 2 epua
10.Acha zipoe kidogo pakua kwenye sahani tayari kwa kula
NB:
1.Hakikisha mchuzi unakua mzito mzito na mdogo
2. Pika ndizi zako kwa moto wa wastani ili zisigande kwenye sufuria
3.Epuka kukoroga wakati wa kuzipika ndizi zako
4.Kama utataka kukoroga chukua tambara safi shika sufuria yako itikise au chukua banio la ugali bana kwenye sufuria na uitikise
Furahia Ndizi Zako.
MAHITAJI
1.Nyama ya kusaga robo
2.Mayai 10
3.Kitunguu maji kikubwa 1
4.Kitunguu thomu punje 5
5.Mdalasini wa unga nusu kijiko cha chakula
6.Uzile(Binzari nyembamba) kijiko 1 cha chakula
7.Pilipili manga nusu kijiko cha chakula
8.Pilipili ya kuwasha 1
9.Chumvi kiasi
10.Mafuta ya kupikia nusu lita
11.Karoti 1
12.Pilipili boga(Pilipili hoho) 1
13.Paprika(sio lazima) nusu kijiko cha chakula
MAANDALIZI
1.Osha vitu vyako vyote vinavyo hitajika kuoshwa
2.Katakata vitunguu maji vidogo vidogo kwa umbo la pembe nne(Square)
3.Para keroti yako kwa kutumia Grater(Kipario)
4.Katakata Pilipili hoho kwa umbo la pembe nne(Square)
5.Twanga kitunguu thomu,chumvi na ndimu
6.Vunja Mayai 3 weka chumvi na uyapige pige na umma
JINSI YA KUPIKA
1.Chemsha mayai 7 na chumvi mpaka yaive
2.Chemsha nyama ya kusaga na chumvi na ndimu
3.Weka karoti,pilipili hoho,kitunguu maji,pilipili uloitwanga,viungo vya unga changanya vizuri
4.Menya Mayai yako kisha yakate kati sehemu mbili sawa
5.Toa viini viweke kwenye nyama ya kusaga na uichanganye vizuri
6.Tengeza nyama yako shape ya duara
7.Weka vile viduara vya nyama kati kati ya yai ulolipasua
8.Weka mafuta jikoni yaache yapate moto
9.Chovya egg kebab zako kwenye mayai mabichi na chovya kwenye karai la mafuta
10.Ziache kwa dakika 3 kisha zigeuze
11.Baada ya dakika 2 zitoe ziweke kwenye chujio au tissue
12.Acha zipoe tayari kwa kula
NB:1.Hakikisha mayai yanaiva vizuri
2.Hakikisha mafuta yanapata moto vizuri kabla kuzichovya ili yai na nyama zisiachane
Furahia Egg Kebab Zako.