Pages

Pages - Menu

Alhamisi, 15 Septemba 2016

JUISI AU MILK SHAKE YA TENDE(DATES MILK SHAKE)



MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Tende 20
 20 Dates

2.Maziwa Glasi 1 na nusu
 1 and 1/2 Glass of Milk

3.Karanga zilosagwa robo kikombe
 Quater Cup of  Crushed Ground nuts 

4.Arki Pine Apple robo kifuniko cha chupa yake
 Pine Apple Essence 1/2 Cap(Caps of Pine Apple Essence Bottle)

5.Maji Ya Uvugu uvugu Kikombe Kidogo 1/2
  1/2 Small Cup of Warm Water


MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Toa kokwa(Mbegu) kwenye tende upate nyama ya tende tu
  Remove the hard pit from dates chop them coarsely

2.Weka kwenye jagi la blenda nyama za tende
 Add them to the jug of blender

3.Mimina maji kwenye blenda acha tende ziroane kwa dakika zipatazo 10
   Pour a cup of water into the blender's jug let the dates be soaked for atleast 10 minutes 

4.Weka maziwa kwenye friza hadi yafanye chenga chenga
  Refrigerate milk until frozen 

JINSI YA KUTENGEZA/HOW TO MAKE
1.Saga Tende zako taratibu mpaka zisagike vizuri
 Blend the soaked dates well till you gets smooth puree

2.Mimina karanga kwenye jagi
 Add crushed ground nuts into the jug

3.Mimina maziwa kwenye jagi lenye tende
 Pour the frozen milk into the jug having date

4.Malizia kuweka arki
 And finally add pine apple essence

5.Saga Mchanganyiko wako taratibu mpaka usagike vizuri
 Blend the mixture well till gets smooth puree

6.Ikichanganyika vizuri mimina kwenye glasi tayari kwa kunywa
 When blended well pour into the glass ready to serve
 
7.Unaweza kuinywa yenyewe au na kitafunio chochote upendacho
 You can serve it with any bite you prefer or drink as it is

Angalizo:Note
1.Usiache maziwa yakaganda hadi kuwa barafu ngumu yakifanya chenga tu inatosha kabisa 
 Do not let the milk frozen complete ,remove in the freezer once started to form the ice  

2.Hakikisha unaondoa kokwa(mbegu) za tende vizuri
 Make sure you remove carefully the hard pit in the dates

Furahia Milk Shake Yako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni