Pages

Pages - Menu

Alhamisi, 4 Agosti 2016

NANGATAI


MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Siagi 250gm
 Butter 250gm

2.Samli 250gm
  Ghee 250gm

3.Sukari Vikombe 2 na nusu
   Sugar 2 1/2 Cups

4.Unga wa Ngano vikombe 10 vilivyojaa
  Plain Flour 10 Cups(Full)

5.Unga wa Semolina vikombe 2 na nusu
  Semolina Flour 2 1/2 Cups

6.Rangi nyekundu kiduchu
  A pinch of Red Colour(Powder)

7.Arki Vanilla vifuniko 2
 Vanilla Essence 2 Caps(Caps of Vanilla Bottle)

8.Baking Powder kijiko cha chai 1
   Baking Powder 1 Tea Spoon

MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Katika bakuli weka samli,siagi pamoja na sukari
  Mix butter,ghee and sugar in a bowl

2.Saga kwa dakika 4 tu mpaka ichanganyike
  Use hand mixer to beat the mixture for 4 minutes only

3.Weka baking powder saga kwa dakika 1
 Add baking powder and keep mixing for 1 minutes

4.Weka vanilla endelea kusaga kwa dakika 1
  Add Vanilla and beat for another 1 minutes

5.Anza kuweka unga wa semolina kisha saga kwa dakika 2 tu
 Add semolina flour then keep beating for 2 minutes

6.Kisha weka unga wa ngano uliochekechwa mpaka ushikane na kuwa donge laini ukishikana tu basi
 Add the sifted plain flour till you get a very soft dough

7.Chukua trea weka karatasi za kuokea au karatasi nyeupe yoyote
 In a baking tray add the baking paper

8.Kata donge dogo weka mkononi fanya upate hilo umbo la duara
  Cut the dough into small dough then make it a circular by using your hand

9.Endelea kutengeza na kisha ziweke kwenye trei
 When you are done keep the cookies in the tray

10.Weka rangi kwenye kikombe tia maji kiduchu changanya na kijiti
 In a cup add the powdered food colour with water and stir it by using a stick 

11.Kisha chukua tone moja la rangi weka kati kati ya nangatai
   With a stick take a drop of the colour mixture and keep at the center of your cookies

12.Washa jiko la kuokea(Oven/Cooker) moto wa 150
 Pre heat or heat the Oven around 150'C

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka nangatai acha ziive kwa dakika 30 tu
 Bake the Nangatai for 30 minutes only

2.Zitoe ndani ya jiko utaziona laini acha zipoe humo humo kwenye trei 
 Remove from the oven let them cool while they are in the tray

3.Acha zipoe kama dakika 5 mpaka 10 
 Let them cool for 5 to 10 minutes

4.Tayari kula na kinywaji upendacho au zenyewe
  You can serve with any drink you prefer
Nimetumia kikopo cha gram 100 cha Blue Band kupimia kila kitu
I use this cup for all measurements 


Angalizo:Note;
1.Usisage sana kama keki fata maelezo nilio yatoa vizuri
  Dont over beat the mixture follow well the instructions i provided

2.Usitengeze pana sana kwani huumuka wakati wa kuzioka
 Make sure the cookies height is not wider since it raises during baking

3.Wacha nafasi baina ya nangatai moja na nyengine zikiwa jikoni hutanuka zikipata moto 
 Leave enough space between one Nangatai and another in the baking tray because they expand when heated

4.Usiweke matone mengi ya rangi kila inapopata moto nalo huongezeka ukubwa
 Don't keep more than one drop at the center of nangatai because the dot size is increasing when heated 

5.Kama jiko lako lina moto mkali basi hakikisha zikibadilika rangi tu uzitoe
 If you can not control the temperature of the your oven remove the nangatai into the oven once they starts to turn into light golden brown colour

6.Usitoe kwenye trei kama hazijapoa zinaweza kuvunjika
 If they are not cool yet don't remove them from the baking tray they can break since they are not cool

Furahia Nangatai Zako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni