MAHITAJI/INGREDIENTS
Mikate/Buns
1.Unga wa Ngano 400gm
400gm Plain Flour
2.Chumvi Kijiko Cha Chakula 1/2
1/2 Tbsp Salt
3.Hamira Kijiko Cha Chakula 1 1/2
1 1/2 Tbsp Yeast
4.Maziwa Kikombe kidogo Cha Chai 1
1 1/2 Tbsp Yeast
4.Maziwa Kikombe kidogo Cha Chai 1
1 Small Cup Milk
5.Sukari Kijiko Cha Chai 1/2
1/2 Tea spoon Sugar
6.Siagi Vijiko Vya Chakula 2
2 Tbsp Butter
7.Kiini cha Yai 1
1 Egg Yolk
8.Unga wa ngano nusu kikombe kwa ajili ya kusukumia
1/2 Cup Flour for rolling out the dough
Samaki/Fish
1.Samaki Nguru Kipande kikubwa 1
1 Large Piece King Fish
2.Pilipili Boga(Pilipili Hoho) 1
1 Green Pepper
3.Keroti 1
1 Carrot
4.Chumvi Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Salt
5.Ndimu zilokamuliwa 2
Lemon juice(2 Lemon)
6.Fish Masala Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Fish Masala
7.Pilipili Manga Kiduchu ya unga
A pinch of Black Pepper powder
8.Kitunguu thomu punje kubwa 1
1 Cloces of Garlic
9.Pilipili ya kuwasha 1
1 Red Chilli
10.Uzile(Binzari Nyembamba) ya unga Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Cumin Powder
MAANDALIZI/PREPARATIONS
Samaki/Fish
1.Osha kipande cha samaki weka kwenye sufuria
Rinse well the piece of fish and keep it in the pan
2.Twanga Pilipili na kitunguu thomu
Grind the mixture of red chilli and garlic
3.Para keroti kwenye kibakuli
Grate a carrot in a separate bowl and keep it a side
4.Katakata pilipili hoho ndogo ndogo
Chop the green pepper in a separate bowl and keep it a side
Mikate/Buns
1.Kwenye Kikombe kitupu changanya Hamira,sukari,unga kijiko 1 na maziwa vijiko 3 acha iumuke
In an empty cup add yeast,sugar,1 Tbsp flour and 3 Tbsp milk and let it rise
2.Kwenye bakuli weka unga chumvi na siagi changanya kwa mkono hadi ichanganyike
In a separate bowl add flour and butter then use your hand to mix them well
3.Kisha mimina hamira ilioumuka changanya vizuri
Pour the raised yeast and keep mixing
4.Mimina maziwa kidogo kidogo mpaka upate donge moja
Pour the milk little by little to get a dough
5.Kanda unga hadi uwe mlainii
Knead the dough till soft
6.Acha uumuke kwenye sehemu ya joto kiasi dakika 40
Leave it for 40 minutes to rise until double or triple in size
7.Ukiumuka kata madonge 5
Then cut into 5 dough
8.Kisha fuata hatua nilizozieleza kwa picha hapo chini
Then follow the below procedures
9.Chovya donge lako kwenye unga mkavu na usukume kwa urefu sio duara kama picha inavyoonekana
Take a dough into plain flour and roll out to get a dough of long shape not circular one as shown at the image above
10.Kisha kunja donge lako kutoka ncha ya mwisho kueleka mwanzoni
Roll the first end towards the last ends
11.Utapata umbo la urefu kama hivyo
You will have this shape
12.Uvute nchani ili likae sawa kama hivyo
Pull each ends to get clear rope shape
13.Chukua kisu chana karibia na nchani mpaka mwisho wa upande wa pili kama linavyo onekana
Use a knife to slice the dough starting nearly to the first end points
14.Kunja upande mmoja kuelekea kati
Bring each ends to the center
15.Malizia upande wa pili kupata umbo la kopa
Bring the other ends to get that heart shape
16.Chota samaki weka katikati ya kopa lako.Jinsi ya kutengeneza samaki nimeelezea chini hapo
Take the fish mixture by using spooon and add the mixture to the center of the heart.I hace explained on how to make fish mixture in cooking part
17.Weka kwenye trei acha yaumuke kwa dakika 10
Put them into the baking tray and let them rise for 10 minutes
18.Piga kiini cha yai kisha yapake
Beat the egg yolk and apply on top of the buns
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
Samaki/Fish
1.Weka ndimu na chumvi kwenye samaki
Add salt and lemon juice into the pan having fish
2.Mchemshe hadi aive abakie na vimaji kiduchu sana
Bring to boil but don't let it dry ,has to be moist
3.Muepue acha apoe kisha mtoe miba
Remove from the stove and let it cool
4.Weka Pilipili na kitunguu ulivyo vitwanga
Add the mixture of garlic
5.Weka na keroti na Pilipili boga kisha changanya vizuri
Add the carrots and green pepper
6.Malizia kuweka Uzile,pilipili manga na fish masala
Then add cumin powder,black pepper and fish masala
7.Endelea kumchanganya vizuri weka pembeni
Mix the mixture very well and keep it aside
8.Onja chumvi kama ipo sawa endelea na hatua nyengine
Check the salt you can add if it is not enough
Mikate/Buns
1.Oka kwa moto wa 150 kwa dakika 30 mpaka 40
Bake the buns for 30 to 40 minutes
2.Yakiiva acha yapoe na yapoe weka kwenye sahani
When they are done let them cool and add to the plate
3.Unaweza kula na Chai,juice au kinywaji upendacho
You can serve with juice or any drinks
Angalizo:Note
1.Unaweza kuweka nyama,mbogamboga au hata mitupu bila ya samaki,nyama au mboga mboga
You can add minced meat or vegetable or nothing on top instead of fish
2.Ikiwa hujaweka chochote ifanye ya sukari badala ya chumvi
If you add nothing on top it is preferable to use sugar during preparation to have sugar taste
3.Hakikisha unga umekandwa hadi kuwa mlaini kabisa
Knead the dough till completely soft
4.Usiipike sana inakuwa migumu ikisha kupiga rangi ya dhahabu itoe
Don't over cook them when they turn into golden colour remove from the oven
5.Usiache ikaumuka kupitiliza baada ya kuweka samaki hupelekea kupoteza umbo lake
Do not let double or triple raised after you add fish on top
Furahia Mikate Ya Kopa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni