MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Muhogo kiasi(kama mitano)
2.Nazi ndogo iliokunwa
3.Nyanya(Tungule) ndogo 2
4.Kitunguu maji kidogo 1
5.Pilipili Hoho(Pilipili boga) 1
6.Keroti 1
7.Pilipiil Mbuzi 1
8.Nyanya ya paket(Tomato paste) kijiko 1
9.Ndimu ndogo 1
10.Chumvi kiasi
11.Maji kiasi
12.Fish Masala kijiko cha chai 1
13.Kitunguu thomu kilotwangwa kijiko cha chai 1
14.Samaki kiasi upendacho
MAANDALIZI/PREPARATION
1.Menya muhogo kata kata vipande vidogo vidogo
2.Ioshe kwa maji safi
3.Weka kwenye sufuria na maji kiasi
4.Weka maji kwenye nazi iliokunwa
5.Chuja tui zito la kwanza
6.Kisha chuja tui la pili jepesi ujazo wa vikombe 3 vidogo vya chai au zaidi
7.Osha viungo vilobakia
8.Katakata vyote kwa pamoja(Kitunguu maji,keroti na pilipili hoho,nyanya)
9.Osha samaki weka kwenye sufuria
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka chumvi kwenye sufuria ya muhogo
2.Weka jikoni acha uchemke mpaka uive na kuwa laini
3.Kamua ndimu na maji kidogo kisha mimina kwenye sufuria yenye samaki
4.Weka fish masala kwenye samaki
5.Iweke jikoni funika kwa dakika moja acha samaki aive kidogo kwa mvuke
6.Malizia kuweka viungo ulivyo vikatakata katika hatua namba 8 pamoja na pilipili
7.Weka nyanya ya paket kisha funika kidogo wacha viive hakikisha samaki hakauki na kuwa mkavu
8.Muhogo ukiiva mwaga maji yote bakisha muhogo mkavu
9.Mimina tui la pili lile jepesi kwenye muhogo
10.Ongeza na chumvi rudisha muhogo jikoni
11.Acha uchemke mpaka tui lipungue kidogo mimina tui la pili
12.Baada ya dakika moja mimina samaki mwenye viungo kwenye muhogo wako
13.Acha kwa dakika 1 nyengine epua
14.Acha upoe kisha toa samaki weka pembeni
15.Chukua mwiko uchanganye vizuri muhogo uchanganyike na vile viungo
16.Pakua sahanini na muweke samaki wako juu ya muhogo tayari kwa kula
Angalizo:Note
1.Hakikisha unatafuta muhogo ambao sio mchungu
2.Usichemshe muhogo mpaka ukaiva sana pia usiuwahishe ukawa haujaiva
3.Tui la pili ukiweka lifunike muhogo kidogo
4.Ukisha kuweka tui la pili usiuache muhogo ukakauka ukakosa rojo rojo
Furahia Muhogo wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni