MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Nyama ya kusaga robo
1/4kg Minced Beef
2.Kitunguu maji kikubwa kiasi 1
1 medium size Onion
3.Vitunguu thomu punje kubwa 3
3 Garlic Cloves
4.Tangawizi kijiko cha chai 1(ilotwanga)
1 Tea spoon minced Ginger
5.Pilipili ya kuwasha 1(au zaidi kama mpenzi wa pilipili)
1 Chili Pepper or more
6.Ndimu 2
2 Lemon
7.Pilipili manga ya unga nusu kijiko cha chakula
1/2 Tbsp Black Pepper
8.Mdalasini wa unga nusu kijiko cha chakula
1/2 Tbsp Cinnamon powder
9.Uzile(Binzari nyembamba) ya unga kijiko kimoja
1 Tbsp Cumin powder
10.Mayai 3
3 Eggs
11.Chumvi kiasi
Salt to taste
12.Mkate wa slice(2) au Boflo 1
2 Slice of bread or Small bread
13.Mafuta ya kupikia nusu lita
1/2 Litre of Cooking Oil
14.Pilipili hoho(Pilipili boga) ndogo 1
1 Green pepper
15.Karoti ndogo 1(ilioparwa)
Grated carrots
16.Unga wa Sembe/wa Mchele robo kikombe
1/4 Cup Maize/Corn Flour
17.Kebab Masala
MAANDALIZI/PREPARATION
1.Twanga kitunguu thomu,pilipili na chumvi na uviweke pembeni
Grind the mixture of red chilli,salt and clove of garlic and keep it aside
2.Menya kitunguu maji,karoti
Peel the onion,carrot
3.Kisha pasua kitunguu maji katikati na kisha kikate kwa urefu
Cut the onion into halves and cut it into slice shape
4.Katakata Pilipili hoho
Chop the Green Pepper
5..Andaa kibakuli vunja mayai mawili weka na chumvi kidogo yachanganye na kijiko au umma na yaweke pembeni
Break two eggs in a small bowl add a pinch of salt and beat them with spoon or folk
6.Kamua Ndimu weka kwenye kibakuli
Squeeze Lemon in a separate bowl to get lemon juice
7.Chukua mkate kama ni wa Boflo toa nyama ya ndani weka kwenye kibakuli roweka na vimaji kidogo acha urowane
Take a bread and remove the crust and soak the crumb(inner white part) in a bowl with water
8.Kama ni slice ondoa ile wekundu wa kuiva unaozunguka slice chukua nyama ya ndani roweka kwenye maji
If you use slice also remove the crust and soak the remaining part into the water
9.Mikate ikirowana ikamue maji yote mpaka ibaki nyama kavu weka pembeni
After some time remove the crumb and squeeze by using your hand till get dried
JINSI YA KUPIKA
1.Weka nyama jikoni tia chumvi,ndimu usiweke maji acha itoe maji yenyewe hadi iwive
In a medium heat cook the minced beef added salt and lemon juice till dry
2.Ikiiva epua nyama acha ipoe
When its ready remove it from the stove and let it cool
3.Changanya nyama yako vizuri weka tangawizi,pilipili manga,mdalasini,uzile na uichanganye vizuri
Then add ginger,black pepper,cinnamon,cumin in the cooked minced beef
4.Weka kitunguu maji,karoti,pilipili hoho ulivyovikata weka kwenye nyama
Add Chopped Onion,Carrot,Green Pepper
5.Weka Kebab masala na uchanganye mchanganyiko wako vizuri
Add Kebab Masala and mix the mixture well
6.Weka nyama za mikate ulioikamua maji na endelea kuchanganya
Add the dried crumb and keep mixing the mixture
7.Malizia kuweka yai moja kwenye nyama changanya vizuri mchanganyiko wako
Break the remaining egg and add into the mixture and continue to mix till combined
8.Chukua nyama yako tengeneza umbo la maduara madogo kiasi mpaka umalize nyama yako.
Take a small portion of a mixture and use your hand to make a round ball like meat balls
9.Weka mafuta kwenye karai yaache yapate moto sana mpaka yatoe moshi
Heat the oil to a maximum
10.Nyunyizia unga wa sembe kidogo sana kwenye kababu zako
Sprinkle the corn flour/maize flour on top of the kebabs
11.Chukua maduara yako yachovye kwenye mayai kisha weka kwenye mafuta
Soak the round balls into the beaten egg and add into the heated oil
12.Ziache dakika 3 kisha zigeuze na ziwache kidogo
Leave for 3 minutes and turn into other side
13.Zikiwa za brown zitoe weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta
When they turn into golden brown remove them and take into sieve or tissue
14.Weka kwenye sahani inapendeza uweke na chatne wakati wa kula
When they get dried serve with chatne(it recipe available in Urojo post)
15.Unaweza kula kababu zako na Chapati au mkate wowote ule.
You can serve with bread,chapati,juice or as they are.
Angalizo:Note
1.Ili kababu zipendeze hakikisha zinachapuka viungo vizuri
Marinate the mixture well to have good taste
2.Mayai ya kuchovyea wakati wa kupikia yawe ya kutosha,unaweza kuwekamaji kidogo ukipenda
Beat an enough egg for soaking the meat balls,you can add little water when needed
3.Wakati wa kuzipika hakikisha mafuta yamepata moto haswaa
Dont cook them if the oil is not heated well
4.Zipike taratibu usizifanyie haraka kuzigeuza hakikisha zinapiga rangi ya brown ndio uzigeuze
Dont turn into other side if the lower side is undone
5.Mafuta yasipopata moto vizuri kababu zinaweza kupasuka kwenye mafuta
If you hurry to cook before the oil get heated well the kebab will break during frying
6.Ikiwa unashindwa kuviringisha kupata duara ongeza mkate wa slice ulioroekwa na kukamuliwa
If you fail to get round ball soak one slice then dried it and add in the mixture till combined
Furahia Kababu Zako
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni