Is a Tanzanian Blog which prepare different food recipes found all over the world.Here you get the chance of reading Swahili and Non Swahili recipes found across the world.The recipes are written by two languages i.e Swahili and English.Welcome all to read and leave your comment about our recipes. Karibuni Nyote mjifunze mapishi ya Kiswahili na mengineo yanayopatikana dunia nzima.Karibuni mjifunze na tunakaribisha maswali na maoni tutakujibu haraka iwezekanavyo. Ahsanteni Sana.
Pages
▼
Pages - Menu
▼
Jumatatu, 9 Mei 2016
KAMBA WA KUKAANGA(FRIED SHRIMPS)
MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Kamba kiasi
Little amount of Shrimps
2.Pilipili Mbuzi iliotwangwa kijiko 1
1 Tbsp minced Red Chilli
3.Ndimu ilokamuliwa vijiko vikubwa 2
2 Tbsp Lemon Juice
4.Chumvi kijiko kikubwa 1
1 Tbsp Salt
5.Kitunguu thomu kilotwangwa kijiko kidogo 1
1 Tbsp Minced Garlic
6.Chicken Masala(Au masala yoyote) kijiko 1
1 Tbsp Chicken Masala(Or Any Masala)
7.Mafuta ya kula Nusu lita
1/2 Litre any Cooking Oil
8.Maji kiasi kwa ajili ya kuoshea kamba
Any amount of Water for Washing shrimps
MAANDALIZI/PREPARATION
1.Osha kamba vizuri kisha waweke kwenye bakuli kubwa kiasi
Rinse well shrimps and keep them in big bowl
2.Waweke vitu vyote nilotaja hapo juu kasoro mafuta
Marinate them by adding all ingredients mentioned above except cooking oil
3.Vaa gloves au jifunge mfuko mkononi wachanganye vizuri mpaka wakolee viungo
Use a glove to mix them well till get marinated
4.Kisha waache kwa dakika 5 mpaka 10 waingie viungo vizuri
Leave them for 5 or 10 minutes
5.Mimina mafuta kwenye karai
Pour some oil in a cooking dish or frying pan
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka mafuta jikoni yapate moto vizuri
Bring the oil to maximum heat
2.Weka kamba utawaona wanabadilika rangi kuwa ya dhahabu
Add the shrimps you will see them turn to gold
3.Waache kwa dakika 3 tu kisha wageuze kwa kuwachanganya
Leave them for 3 minutes then turn the shrimps upside down by mixing them
4.Subiri dakika 3 nyengine waepue weka kwenye chujio wachuje mafuta
Wait for another 3 minutes and remove them from the oil to the sieve or colander to let the shrimps drain
5.Subiri wapoe waweza kula wenyewe au na wali,mkate n.k
Let them cool and they are ready to serve alone or with cooked rice,breads and so on.
Angalizo:Note
1.Usiwaweke kwenye karai kama mafuta hayajapata moto vizuri
Do not add them if the oil is not full boiled
2.Pika kwenye mazingira safi wakiingia mafuta ya taa wanabadilika ladha na kuwa na ladha ya mafuta ya taa
Keep kerosene far away during cooking them cause it changes the taste when contaminated
3.Unaweza kutoa maganda kabla ya kuwapika,wakati wa kuwala au unaweza kula na maganda yake
You can peel the shrimps before or after cooking or you can serve them without peeling them
Furahia Kamba Wako
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni